KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, July 25, 2014

Lil Wayne aingia kwenye michezo na kumvuta Cristiano Ronaldo kwenye madili ya fedha nchini Marekani

Cristiano Ronaldo anatarajiwa kuwa mshirika wa kwanza wa Rapa mashuhuri nchini Marekani Lil Wayne katika kampuni yake mpya inayoshughulika michezo nchini Marekani.
Ronaldo nyota wa Ureno si kama ataachana  na kampuni yake ya sasa isipokuwa Lil Wayne atakuwa anahusika na mipango yote inayo muhusu Ronaldo ndani ya Marekani.
Kwa mujibu wa TMZ, ni kwamba Lil Wayne atakuwa anasimamia kila kitu ikiwa ni pamoja matangazo na masoko na utiaji saini wa dili zote zinazomuhusu Ronaldo ndani ya nchi hiyo pamoja na mambo ya modeling.'
Capitalising: Cristiano Ronaldo is looking to market himself more in America
Cristiano Ronaldo ni kama anaonekana anapata soko sana nchini Marekani.

'Weezy (Lil Wayne) amekuwa anataka kuingia katika usimamizi wa mambo ya michezo kwasasa na ana muangalia Ronaldo kama mshirika wake wa kuanza naye kwakuwa ni nyota mkubwa lakini pia ni rafiki yake mkubwa.'
Kwasasa mpira wa miguu umeanza kupata umaarufu mkubwa nchini humo kufuatia mafanikio ya timu ya taifa ya Marekani katika kombe la dunia hivi karibuni, ambapo vituo vya Televisheni vilikuwa vikionyesha fainali zilizopita mwanzo mwisho.