Ridhiwani Kikwete mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa jengo la klabu ya Yanga la mtaa wa Mafia kariakoo jijini Dar es Salaam. |
Mwenyekiti wa klabu ya Yusufu Manji hii leo ameteua Ridhiwani Kikwete kuwa mwenyekiti wa kamati ya kuendeleza ujenzi wa jengo la klabu hiyo lililopo mtaa wa Mafia Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Uteuzi huo umefanyika makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani ambapo Ridhiwani anatakiwa kuteua wajumbe wengine wa kusaidiana naye katika kusimamia ujengo wa jengo ambalo kwa kipindi lilikuwa kama limesahaulika.
Pamoja na mambo mengine Ridhiwani amekabidhiwa hali ya kiwanja na jengo hilo kwa ajili ya kusimamia vema zoezi hilo.
Akiongea wakati akimtangaza Ridhiwani kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo, mwenyekiti wa Yanga Manji amesema anaamini pia kwakuwa Ridhiwani ni mwanasheria hivyo matatizo ya mikataba ya wapangaji wa jengo hilo yatashughulikiwa vema.
No comments:
Post a Comment