KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 14, 2014

Mahakama ya michezo Uswiz yampa angalau ahueni Luis Suarez

Adhabu ya Luis Suarez ya kumng'ata Giorgio Chiellini imepata ahueni kutoka CAS.
Zuio la mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay Luis Suarez lililotokana na kumng'ata mlinzi wa timu ya taifa ya Italia Giorgio Chiellini limepata ahueni kutoka kwa mahakama ya kimichezo ya kimataifa CAS (Court of Arbitration for Sport), ingawaje atakuwa bado akiendelea kutumikia adhabu ya kusimama michezo aliyofungiwa na shirikisho la soka duniani FIFA.

Rufaa ya mshambuliaji huyo mpya wa Barcelona dhidi ya adhabu hiyo imesitishwa mchana wa leo, lakini ahueni imepatikana kwake kwa kuruhusiwa angalau kushiriki mazoezi na klabu yake mpya ya Barcelona.

Taarifa zinasema maelezo zaidi ya kile kilichotokea katika kusikilizwa kwa shauri hilo huenda yakatolewa baadaye.

Suarez, ambaye aliihama Liverpool na kujiunga Nou Camp mwezi uliopita kwa mpango wa uhamisho uliogharimu pauni milioni £75, atasalia katika  adhabu ya kusimama michezo ya klabu yake mpaka mwezi Oktoba, adhabu ambayo itamfanya kukosa michezo nane ya La Liga na mingine mitatu ya ligi ya mabingwa Ulaya, lakini klabu ya Barcelona imepata nafuu kwani sasa ataungana na wenzake kushiriki mazoezi ambayo yatamuweka katika hali nzuri kiuchezaji kabla ya mchezo wake wa kwanza dhidi ya Real Madrid.