Meneja mpya wa Sunderland Paolo Di
Canio amekataa kujibu swali aliloulizwa kuhusiana na kama anaikumbatia imani
yake ya kifashisti katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari akiwa
bosi mpya wa Sunderland.
Bosi huyo mtaliano ameelezea juu ya
gumzo kubwa lililoibuka juu ya kuteuliwa kwake kuwa meneja wa Sunderland akichukua
nafasi ya Martin O’ Neil kuwa ni jambo la kuchekesha na pia la kusikitisha.
Kuhusina na kujiuzulu kwa katibu wa
zamani na makamu wa mwenyekiti David Miliband amesema hili ni jambo la kisiasa
na kwamba hakuwa na majibu juu ya swali hilo.
Di Canio alikataa kuzungumzia juu ya
siasa huku akisema kuwa yeye si mwanasiasa na hayuko bungeni kujibu mambo hayo
na kwamba angeweza kujibu maswali yanayo husu soka.
Di Canio aliripotiwa katika mahojiano
na shirika la habari la Ansa mwaka 2005 kuwa saluti aliyopiga wakati huo
akichezea Lazio ilikuwa ni maalum kwa watu wake ambao walikuwa wakimfuata Benito
Mussolini ambaye alikuwa akiongoza harakati za mafashisti na kwamba halikuwa kwa lengo la ubaguzi.
No comments:
Post a Comment