KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, January 2, 2013

R.I.P SAJUKI.

MSANII wa filamu hapa nchini, Juma Kilowoko, maarufu kwa jina la Sajuki, amefariki Dunia leo saa moja asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
 Sajuki amekufa huku akiwa na kumbukumbu za kuanguka mwishoni mwa mwezi Desemba mkoani Arusha, alipokwenda kufanya shoo, akiizungumzia kama kujichanganya kwa ajili ya kutafuta fedha za kumpeleka tena India kupata matibabu.
 
 Akizungumza mapema leo, Katibu wa Baraza la Filamu Tanzania (TAFF), Wilson Makubi, amesema habari za kifo chake zimeanza kusambaa tangu saa moja asubuhi, hivyo wadau na mashabiki wake watapewa utaratibu juu ya msiba wa msanii huyo mwenye mafanikio katiika tasnia ya filamu Tanzania.
 
 “Sajuki ni msanii mahiri na amekufa katika siku ya pili ya mwaka huu mwezi Januari, hivyo hakika ni pengo kwa wasanii wote pamoja na mashabiki kwa ujumla, ukizingatia kuwa tulikuwa na mapenzi naye.
 
 “Watu walishajichanga kwa ajili ya kumpeleka India msanii huyo jambo ambalo lilifanikiwa kwa dhati, hata hivyo jitihada hizo Mungu ameona amchukuwe kiumbe wake kwa ajili ya maisha ya milele,” alisema.
 Kifo cha Sajuki kwa wasanii kimefungua dimba kwa mwaka 2013, huku ukiwa na kumbukumbu za kuondokewa na wasanii watano katika kipindi cha mwaka 2012, akiwamo Steven Kanumba, Sharomillionea na wengineo.

No comments:

Post a Comment