Makamu wa kwanza wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad anatarajiwa kufungua rasmi michuano ya kombe
la mapinduzi inayotarajiwa kuanza rasmi hii jioni ya leo ambapo michezo miwili itapigwa
katika uwanja wa Aman huko Zanzibar.
Katika mchezo wa kwanza Bandari watakuwa wakikutana na
Tusker ya Kenya na mchezo wa usiku ambao hasa ndio wa uzinduzi utakuwa ni kati
ya Simba na Jamhuri ya Pemba.
Maalimu Seif amealikwa na waandaaji wa michuano hiyo ambayo
bingwa wake mtetezi ni Azam FC ya jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuelekea kusheherekea miaka 49 ya
mapinduzi ya Zanzibar michuano ambayo pia hufanyika kila mwaka .
Akiongea na Rockersports msemaji wa kamati ya maandalizi ya michuano hiyo Farouk Karim amesema,
Tayari timu za Tusker, Jamhuri ya Pemba na Simba zimekwisha kuwasili
Zanzibar tangu jana na taarifa zinasema Azam , Coast Union na Mtibwa zinatarajiwa kuwasili
huko hii leo . Tiketi zilizo arifiwa mapema kuwa zinatengenezwa nje ya nchi zimeshawasili na zimetoka nje ya nchi.
Forouk ametaja viingilio kuwa ni kwa mchezo wa kwanza jukwaa la Urusi 1000,mzunguko 2000, VIP 5000. Usiku 2000, 3000,
VIP 10000.
No comments:
Post a Comment