Mancini: Balotelli ni muhimu kwa
mmiliki wa klabu.
Roberto
Mancini amesisitiza kuwa Mario Balotelli atasalia katika klabu yake ya Manchester
City kufuatia mmiliki wa klabu Sheikh Mansour kumsajili mtaliano huyo kutokana na kile alichokiita kama
uwekezaji mkubwa katika klabu hiyo.
Balotelli hajaonyesha
kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu, ambapo amefunga magoli 3 tu katika mashindano
yote, jambo ambalo lilianzisha minong’ono ya chini chini kuwa mshambuliaji huyo
huenda akaondoka ligi kuu ya England ‘Premier League’ na kuelekea Italia ‘Serie A’ kwa
kigogo cha soka nchini humo AC Milan mwezi huu wa January.
Hata hivyo
meneja Mancini ameweka wazi kuwa’
"Sheikh
Mansour anampenda Balotelli kwakuwa anaamini anakipaji na analitangaza jina la City
duniani"
"tunapaswa
kukubali kuwa Mario alisaini kama uwekezaji mkubwa, na hii si klabu ambayo
inatupa mtaji wake kupitia dirishani
"nadhani
Mario atasalia lakini huko baadaye itategemea na yeye mwenyewe"
Redknapp amethibitisha kumtaka Joe Cole.
Bosi wa Queens
Park Rangers Harry Redknapp amethibitisha kuwa ataongea na meneja wa Liverpool Brendan Rodgers kuhusiana na usajili wa Cole.
Redknapp anamjua
vema Cole tangu wakati huo wakiwa pamoja katika klabu ya West Ham, na baadaye
kufanya vema katika timu ya taifa ya England.
Cole alikuwa
katika mpango wa Redknapp tangu wakati huo akifundisha Tottenham, lakini kiungo
huyo akaamua kuelekea kwa meneja Roy Hodgson katika klabu klabu ya Liverpool ambako
bado hajafanikiwa kuonyesha mafanikio.
Leonardo akanusha mazungumza na Ashley Cole.
Mkurugenzi wa
michezo wa Paris Saint-Germain, Leonardo amepuuza taarifa kuwa yuko katika
jaribio la kumshawishi Ashley Cole aondoke Chelsea katika dirisha hilo dogo
lililoanza hii leo barani ulaya.
Cole atakuwa
huru baada ya mkataba wake kumalizika Stamford Bridge mwishoni mwa msimu na bosi wa
sasa Rafael Benitez alinukuliwa akiweka wazi katika moja ya mikutano yake na wandishi wa
habari kwamba mlinzi huyo wa England ataondoka darajani majira ya kiangazi.
Hata hivyo
baadaye alirekebisha kauli yake na kusema kuwa Cole ataendelea kusalia Chelsea mara
baada ya mkataba kumalizika jambo ambalo si Cole mwenyewe wala Frank Lampard
ambaye naye yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake aliyekubaliana na
masharti mapya ya kusalia hapo.
Kwasasa PSG
ambayo inafanya kufuru kifedha katika matumizi ya usajili inanolewa na Carlo
Ancelotti, ambaye huko nyuma alikuwa pamoja na Cole wakati huo akiifundisha Chelsea.
Leonardo pia
amekanusha taarifa kuwa Wesley Sneijder anampango wa kujiunga PSG ambapo amesema
katika nafasi yake tayari PSG inawachezaji watano
Hata hivyo
klabu hiyo ambayo kwasasa inamilikiwa na wamiliki wapya wa Qatar Investment
Authority, imeanzisha mpango wa kumtaka Lucas Moura akitokea Sao Paulo ambaye
tayari ameshakubali kujiunga nao na huenda wengi wakafuata.
Cudicini aamua kuelekea Galaxy.
Mlinda mlango
wa Tottenham goalkeeper Carlo Cudicini ameamua kujiunga na LA Galaxy
inayoshiriki ligi ya soka ya nchini Marekani MLS kwa mkataba wa miaka miwili.
Cudicini, mwenye
umri wa miaka 39, alishindwa kurejea katika ubora wake wa kunyaka mipira kule White
Hart Lane baada ya kupata ajali ya pikipiki ambayo ilimtengua kiuno na maumivu
makali yaliyotona na kuumia mfupa wa nyonga.
Kufuatia kusajiliwa
kwa Hugo Lloris na kupelekea yeye kuwa mlinda mlango namba tatu nyuma ya mlinda
mlando mfaransa Brad Friedel ambaye hivi karibuni amesaini mkataba mpya, sasa
Cudicini ameamua kutafuta mwelekeo mpya nchini Marekani.
Mtaliano huyo
ameamua kuondoka kusaka namba nchini Marekani na inaarifiwa kuwa anakuwa
ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mshahara mnono.
Cudicini alijiunga
White Hart Lane mwezi January 2009 kwa uhamisho huru baada ya kuidakia Chelsea miaka
tisa na sasa anajiunga na mchezaji mwenzake wa zamani wa Tottenham Robbie Keane katika klabu ya Galaxy.
Walcott: hatma yangu itafahamika hivi
punde.
Theo Walcott
ameelezea juu ya hitajio lake la kutaka kusalia katika klabu yake ya Arsenal licha
ya mshambuliaji huyo sasa kuwa anaweza kufungua mazungumzo na klabu nyingine.
Makataba wa Walcott
wa sasa utafikia kikomo mwishini mwa msimu huu ambapo kwasasa majadiliano juu
ya mkataba mpya yakitazamiwa kuanza baadaye mwezi huu.
Meneja wa Arsenal
Arsene Wenger ana matumaini kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England atafuata
nyayo za wachezaji wenzake vijana wa England Jack Wilshere, Alex
Oxlade-Chamberlain, Aaron Ramsey, Kieran Gibbs na Carl Jenkinson ambao
walisaini mikataba mipya muda kabla ya sikukuu ya Christmas.
Hata hivyo Wenger
amesema mwezi uliopita alitarajia mambo hayo yangekuwa yamemalizwa kabla ya
mwaka mpya.
Licha ya
songombingo hiyo, bado Walcott anasisitiza kuwa anataka kusalia Emirates
Stadium.
Amenukuliwa na
The Sun akisema
“nina imani
kila kitu kitakwenda vizuri hivi karibuni"
“siku zote
nimekuwa nikisema kuwa nataka kusalia na kufurahia kucheza katika timu hii. Hebu
tuone nini kitafuata”
Kwa mujibu
wa sheria za uhamisho ni kwamba kwasasa Walcott anaweza kusaini mkataba wa awali na
klabu nyingine yoyote ya nje ambayo atapenda mpaka mkataba wake utakapo kwisha
rasmi mwezi June ambako ambako atasaini kama mchezaji huru.
No comments:
Post a Comment