KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, July 6, 2012

KOCHA MPYA YANGA AINGIA MKATABA MIAKA MIWILI.

Kocha wa Yanga Saintfiet
                                                               
KOCHA mpya wa timu ya soka ya Yanga, Tom Saintfiet kutoka Ubelgiji amesaini mkataba wa miaka miwili ambao anaweza kuongezwa kamaataipa mafanikio timu hiyo yenye maskani yake katika mtaa wa Twiga na Jangwani.
Akizumza katika hafla ya kutiliana saini mkataba huo Saintfiet amesema kazi yake kubwa aliyonayo ni kuhakikisha timu hiyo inatetea ubingwa wake wa michuano ya Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza baadae mwezi huu.
Kocha huyo ameendelea kusema kuwa anataka kuifanyaYanga ifike mbali na kupata mafanikio katika ligi ya nyumbani lakini pia iweze kufanya vizuri katika michuano mbalimbali ikiwemo ligi kuu ya Tanzania bara na kuwa tishio kwa vilabu vingine vya Afrika kama ilivyo kwa klabu ya TP Mazembe na klabu nyinginezo.
Amesema kitu cha msingi kwa sasa ni mashabiki pamoja na viongozi wa klabu hiyo kumpa ushirikiano ili kwa pamoja waweze kujenga kikosi imara na chenye ushindani katika kipindi ambacho atakuwa kocha kwenye klabu hiyo.
Kwa upande wake katibu wa klabu hiyo John Celestine Mwesigwa amesema mataba wa Thom ni wa kuanzia lakini unaweza kuongezeka kutegemeana na mafanikio ya kocha huyo ndani ya  klabu hiyo.
Hafla ya utiaji saini kwa kocha huyo mbali ya kuwepo kwa viongozi wengine mbalimbali na wanachama waandamizi kama vile Seif Abdalah magari imehudhuriwa pia na makocha wasaidizi Fred Felix Minziro na Mfaume Athumani ambaye kocha wa makipa.
Picha za zoezi la utiaji saini fuatilia mtandao huu.

No comments:

Post a Comment