KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, May 27, 2014

Nyanda Shabani Kado afungua mazungumzo na klabu mbalimbali na kwamba yuko huru

Shabani Kado anasema yuko huru
 Mlinda mlango wa Shaaban Kado amesema yupo tayari kuzungumza na klabu yoyoten ambayo itaonyesha nia ya dhati ya kumsajili katika kipindi hiki cha kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ya soka Tanzania bara

Shaaban Kado ambaye alishuhudia nusu ya msimu wa mwaka 2013-14 uliofikia tamati April 19, akiwa nje ya uwanja kufutia majeraha ya mkono yaliyokuwa yakimkabili, amesema ameamua kufungua milango ya kuzungumza na viongozi wa klabu yoyote kutokana na mkataba wake na uongozi wa klabu ya Costal union kufikia kikomo.

Kado pia amaezungumzia maendeleo ya mazoezi mepesi anayoendelea kuyafanya baada ya kupona jeraha la mkono ambapo amesema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri na kwamba ana matumaini ya kufanya vizuri msimu ujao bila kujali ni katika klabu gani itakayo msajili.
Shabani Kado akichagua Gloves nchini Oman wakati wa ziara ya klabu yake ya Coastal wakati wa mapumziko ya nusu msimu