KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, May 27, 2014

Thomas Mashali amaliza na Promota Alli Mwazoa sasa kupanda ulingoni dhidi ya Kalama

Thomas Mashali akipongezwa na mbunge wa kinondoni Iddi Azzan
 Baada ya mvutano wa muda mrefu bondia Thomas Mashari amefikia makubaliano na prommota Ally Mwazoa kwa kukubalia kupanda ulingoni wakati wowote kwa kuheshimu mkataba waliotiliana saini miezo miwiwli iliyopita.

Thomas Mashari amezungumza na Rockersports na  kuweka bayana makubaliano waliyofikiwa na Promota huyo kutoka jijini Tanga ambapo amesema kwa sasa hana budi kuanza maandalizi ya kupambana na bondia yoyote atakaepangiwa nae, baada ya kuuguza majeraha yaliyosababishwa na ajali ya gari.

Mashali Kulia akitupiana makonde na Meddy Sebyala wa Uganda Oktoba 14 2012 ukumbi wa Friends Corner Manzese jijini Dar es Salaam ambapo alishinda kwa pointi.
Amesema alipishana kauli na Ally Mwazoa kutokana na baadhi ya watua mbao hawapendi ukaribu uliopo baina yao, hivyo kwa juhudi zake pamoja na watu wa karibu wamefanikisha makubaliano waliyoyafikia.

Hata hivyo Thomas Mashari ameweka bayana kumuhitaji kwa udi na uvumba bondia Karama Nyilawila katika pambano ambalo atacheza chini ya Promota Ally Mwazoa.
Mashari amesema anatamani kukutana na Karama Nyilawila kutokana na bondia huyo kuzungumza maneno mengi dhidi yake, halia mbayo inampandisha hasira kila kukicha.

No comments:

Post a Comment