Uongozi wa klabu bingwa nchini Simba umesema kuwa unaendeleea vizuri na maandalizi ya mchezo wao wa kwanza dhidi ya timu kutoka nchini Angola ya Libolo.
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo kwa vyombo vya habari imesema meendeleo ya kambi na mazoezi yao
mjini Arusha yanakwenda vizuri.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga imesema hali ya kikosi ni nzuri morali ya wachezaji iko juu na hakuna
mgogoro au matatizo yoyote.
Paulo Ngalema. |
Majeruhi
mpya ni mchezaji Paulo Ngalema ambaye aliumia goti katika mechi ya juzi dhidi
ya Oljoro JKT. Mchezaji huyo tayari amesafirishwa kurejea Dar es Salaam kwa
ajili ya kufanyiwa vipimo na uchunguzi zaidi.
Kutokana
na tatizo hilo, Ngalema hataweza kucheza katika
ijayo dhidi ya Libolo ya Angola
katika Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi ijayo.
Kupitia taarifa hiyo uongozi
wa Simba umewataarifu wapenzi na washabiki wake kwamba hali ya timu ni
shwari kabisa. Hakuna mchezaji yeyote aliyefungiwa wala kusimamishwa na hakuna
mitafuruku baina ya wachezaji na makocha au wachezaji na viongozi wa klabu.
Simba SC pia inakanusha taarifa zozote za wachezaji wake au makocha
wake kupigwa (au kutaka kupigwa) mara baada ya mechi ya Arusha.
Kwa waliokuwapo
katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta siku ya Jumamosi mara baada ya mechi
dhidi ya Oljoro, watakuwa mashahidi kwamba baadhi ya wachezaji wa Simba
walibebwa na washabiki na Mrisho Ngassa alipewa zawadi ya Sh 10,000 na shabiki
mmoja kutokana na mchezo wake.
Washabiki
walifahamu kuwa matokeo yale ya 1-1 yalikuwa ni sehemu ya mchezo.
Taarifa za
kuwapo kwa vurugu zimetiwa chumvi kwa sababu ambazo klabu yetu haizifahamu.
Simba SC inaomba washabiki wake wawe watulivu na werevu katika
wakati huu ambapo tunajiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Umoja wa
washabiki ndiyo utakaosaidia na si mtengamano.
No comments:
Post a Comment