Chelsea
hatimaye imemteua Roberto Di Matteo kama meneja wake wa kudumu kwa kutiliana
saini mkataba wa miaka miwili.
Di Matteo
aliwekwa kama kocha wa mda kufuatia kutimuliwa kwa Andre Villas-Boas mnamo
mwezi Machi, na akaweza kuiongoza klabu hio akifanikiwa kuifikisha na kushinda
fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na vilevile kombe la FA la England.
Meneja huyo aliyekua kiongozi wa MK Dons na pia West Brom, Di Matteo alipoteza mechi tatu tu kati ya mechi 21 alizosimamia, na kutokana na hali hiyo wachezaji wengi wa klabu waliunga mkono ateuliwe kama meneja wa kudumu hususan baada ya kushinda kombe lililoikwepa klabu hio kwa mda mrefu la Mabingwa wa Ulaya
No comments:
Post a Comment