Kutoka kushoto ni mwenyekiti wa vilabu, mkurugenzi wa ufundi wa tff Sunday Kayuni na mkurugenzi wa fedha TFF Silas Mwakibinga. |
Deni kubwa la kodi linalo tokana na makocha wa timu ya taifa tangu mbrazil Marcio Maximo, Jan Poulsen na Kim Poulsen la zaidi ya shilingi milioni 150 limeigharimu amana za fedha za shirikisho la soka nchini TFF ikiwemo pia amana inayotunza pesa za vilabu vya ligi kuu katika benki ya NMB ambapo kwasasa amana hizo imezuiliwa na mamlaka ya mapato nchini TRA kupitia benki hiyo ili kufidia deni la kodi liliachwa na makocha hao.
Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la soka nchini Sunday Kayuni amesema licha ya jitihada za shirikisho la soka nchini TFF za kuwasiliana na kuikumbusha serikali kupitia wizara ya habari utamaduni na michezo juu ya deni hilo, majibu ilikuwa ni wasubiri serikali inashughulikia.
Amana ya fedha iliyozuiliwa ya vilabu vya ligi kuu ambayo hutumika kama pesa za kujikimu katika ligi kwa vilabu ikiwemo usafiri na malazi ilikuwa katika benki ya NMB ambapo kuzuiliwa kwake kutaathiri kwa namna moja ama nyingine vilabu hivyo.
Kayuni amesema kimsingi wanaishukuru serikali ya awamu ya nne kwa kujitolea kuwalipa makocha wetu wa kigeni kufundisha timu za taifa na kwamba wangeiomba serikali pia iingilie kati kuokoa amana hizo zilizozuiliwa kwani hilo limetokea kutokana na kucheleweshwa kulipwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja wa vilabu Saidi Mohamed amesema kitendo cha kuzuiliwa kwa amana hiyo kimewasikitisha sana kwani deni linalo daiwa na mamlaka ya mapato Tanzania TRA halivihusu vilabu ni deni la malimbikizo ya kodi ya waliokuwa makocha wa timu ya taifa Maximo na Poulsen lakini amana( account) iliyozuiliwa inatunza fedha za vilabu na si pesa za TFF.
Akitoa ufafanuzi juu ya deni hilo mkurugenzi mtendaji wa TFF Silas Mwakibinga amesema kilichotokea kimeishtua ofisi yake, kwani jukumu la kulipa makocha wa kigeni ambao wamekuwa wakiletwa nchini na serikali ya awamu ya nne ni la serikali kupitia wizara ya habari, utamaduni na michezo licha ya kwamba kocha huyo anaajiriwa na TFF, hivyo basi haikuwa sahihi kuzuiliwa kwa amana hizo.
No comments:
Post a Comment