Kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini Tanzania TFF imesema uchaguzi wa chama cha waamuzi FRAT uliofanyika tarehe 17 novemba 2012 mjini Dodoma ni batili kwa kuwa haukuzingatia kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF na maagizo ya TFF.
Kauli ya kubatilisha uchaguzi huo imetolewa leo jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa kamati hiyo Deogratius Lyato katika mkutano wake na waandishi wa habari makao makuu ya shirikisho la soka nchini TFF.
Lyato amesema maamuzi hayo yamezingatia kamati yake kubaini na kujiridhisha kuwa kulikuwepo na ukiukwaji wa katiba ya chama cha waamuzi nchini FRAT na kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF kwa kiwango kikubwa ambao ulifanywa na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya FRAT bwana Muhidini Ndolanga akishirikiana na mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya FRAT na siyo kamati nzima ya uchaguzi ya FRAT.
Amesema kwa kutotimiza wajibu wake wa kusimamia mchakato wa uchaguzi wa FRAT kwa weledi na kutokuzingatia maagizo ya TFF, kamati ya uchaguzi ya TFF kwa mamlaka yake yaliyoanishwa katika katiba ya TFF ibara ya 49(1), kanuni za uchaguzi za TFF ibara ya 6 na 25(6), kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF ibara ya 26(2) na (3) kamati yake imeamua kumuondoa Alhaji Muhidini A. Ndolanga kwenye kamati ya uchaguzi ya FRAT na kuagiza kamati ya utendaji ya FRAT kuteua mtu mwingine kujaza nafasi hiyo.
Lyato amesema kuwa kamati yake ya uchaguzi ya TFF imeamua kuchukua hatua za kikanuni zilizo ainishwa kwenye kanuni za uchaguzi ibara ya 26(8) kumweleza katibu mkuu wa TFF kuwasilisha kwenye kamati ya nidhamu ya TFF ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi uliofanywa na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya FRAT kwa hatua za kinidhamu.
Pia amesema wagombea watatu ndugu Omari Abdulkadir, Sudi Abdi na Khegula Ruvu Kiwanaga ambao walishiriki uchaguzi uliofanyika tarehe 17 novemba 2012 huku wakiwa wazi walikwisha kuondolewa kwenye uchaguzi wa FRAT kwa kukosa sifa, wafikishwe kwenye kamatik ya nidhamu ya TFF kwa mujibu wa ibara ya 26(8) ya kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF kwa hatua za nidhamu.
Amesema mchakato wa uchaguzi wa FRAT haujafutwa na uchaguzi FRAT utafanyika kwa tarehe itakayo pangwa baada ya kukamilika maandalizi ya uchaguzi huo kabla ya uchaguzi mkuu wa TFF na utawahusisha wagombea waliomba uongozi na kukidhi matakwa ya katiba ya FRAT na kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.
Omari Abdulkadir aliuondolewa katika mchakato wa uchaguzi kutokana na kukosa sifa baada ya kutokutimiza masharti ya kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF ibara ya 10(4) ambayo inataka wagombea kujaza fomu za maombi ya uongozi(form no 1) na kusaini fomu hizo kuthibitisha maelezo yako, ambapo kamati ya uchaguzi ya TFF ilibaini fomu hiyo hakujaza Abdulkadir na wala saini haikuwa yake.
Kwa upande wake Sudi Abdi kulijitokeza mkanganyiko katika maelezo yake kwani kamati ilibaini maombi yake ya kugombea nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu wa TFF hayakutimiza masharti ya kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF ibara ya 10(4)
Kamati ilibaini ilibaini kuwa siyo yeye aliyeomba na aliyesaini kwenye fomu yake ya maombi ya uongozi bali fomu yake ilisainiwa myu mwingine sambamba na utata katika maelezo yake ya elimu ya sekondari
Maelezo ya Sudi yanaonyesha kuwa alimaliza elimu ya sekondari mwaka 1990 akiwa na umri wa miaka 28, lakini cheti chake kinaon yesha kuwa alimaliza elimu hiyo mwaka 1979 akiwa na umri wa miaka 17.
Kwa upande wake Ruvu Kiwanga naye hakutimiza masharti ya kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF ibara ya 9. Kamati ya uchaguzi ilibaini kuwa maelezo yake kwenye fomu ya maombi uongozi (form no 1) yana utata.
Kwenye fomu namba 1 anaonyesha kuwa alianza elimu ya kidato cha kwanza katika shule ya sekondari vituka mwaka 1991 akiwa na umri wa miaka 29 na kumaliza mwaka 1994 akiwa na umri wa miaka 32.
Pamoja na hilo pia nakala za cheti cha mafunzo ya waalimu wa mpira wa miguu alichotunukiwa na shirikisho la soka Afrika CAF inakinzana na maelezo ya muda aliosoma sekondari.
No comments:
Post a Comment