KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, November 23, 2012

MAVETERANI WA KANDA YA ZIWA WAPELEKA MASHABIKI NCHINI UGANDA KUZISHANGILIA TIMU ZA TAIFA. AKINA USINIUMIZIE KUINGIA BURE MICHEZO YA TIMU YA TAIFA YA UGANDA 'THECRANES'.



 
Umoja wa wanamichezo waliowahi kuchezea klabu mbalimbali za ligi kuu mkoani Kagera (Bukoba Veteran Sports Club) umeamua kuwapeleka mjini Kampala mashabiki 60 kwenda kuishangilia timu za taifa za Tanzania Bara maarufu The Kilimanjaro Stars nu kama Zanzibar Heroes wakati wa michuano ya kombe la Chalenji.

Mashabiki hao wanatokea katika mikoa ya kanda ya ziwa ambapo kundi la kwanza litaondoka jumapili novemba 25, 2012 kuwahi mchezo wa kwanza wa Kilimanjaro Stars dhidi ya Sudan Kaskazini.

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa Bukoba Veterani Shija Richard amesema lengo kubwa ni kuhamasisha wachezaji wa timu za Tanzania zote mbili kwenye michuano hiyo mikubwa ya mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kutoa hamasa kwa watanzania kujenga tabia ya kushangilia timu zao. 

Amesema tayari taratibu zote zimeshafanyika ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) ili wawasiliane na mamlaka zinazohusika kwa ajili ya kupatiwa eneo maalumu uwanjani litakalowezesha watanzania waweze kuishangilia vizuri timu ya taifa.
 
"Tunatarajia kwenda uwanjani na zaidi ya mashabiki 60 ambao hivi sasa wanakamilisha taratibu za mwisho za kuvuka mpaka wa nchi."

"Matarajio yetu ni kuendelea kuziunga mkono timu za taifa katika 
michuano hiyo hadi kufikia mwisho wa michuano. Tunaomba watanzania wengine walioko kanda ya ziwa katika mikoa ya Shinyanga, Mara na Mwanza watuunge mkono"


Shirikisho la soka kwa nchi za Afrika Mashariki na kati CECAFA kwa kushirikiana na shirikisho la soka nchini Uganda FUFA limetangaza wanawake kuingia bure katika michezo yote ambayo timu ya Taifa ya Uganda 'The Cranes' itakapo kuwa inacheza michezo yake, hivyo hatua hiyo ya Bukoba veterans inaonekana ni ya kuungwa mkono katika jitihada ya watanzania kuongezahezaji wa timu zote mbili.

Wakati huohuo timu za mataifa ya Burundi, Rwanda, Malawi, Ethiopia, South Sudan, Kenya na Sudan zote mbili zimeshawasili nchini Uganda tangu jana tayari kwa kuanza michuano hiyo wakati ambapo Kilimanjaro Stars ikitarajiwa hii leo.

No comments:

Post a Comment