Kiungo wa Real
Madrid Xabi Alonso amesema hana urafiki wowote na Cristiano Ronaldo lakini ni
watu ambao wanaheshimiana.
Tangu kuanza
kwa msimua kulikuwepo na tetesi zinazo husiana na mahusinao ndani ya kambi ya
Madrid ambapo baadaye Ronaldo akaibuka mbele ya umma na kuweka wazi juu ya
anavyokosa raha ndani ya klabu hiyo.
Kiungo huyo
wa zamani wa Liverpool ndiye mchezaji wa hivi karibuni kunukuliwa akiweka wazi hali
ya ukaribu wake na mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United na kusema
wazi kuwa urafiki wake na Ronaldo haundelei nje ya uwanja.
“baina yangu
mimi na yeye ni watu ambao tuna heshimiana na kila mmoja kumkubali mwenzake ”
“wazi kabisa
si kila mtu ni rafiki yangu nje kambi na pengine huko nje ni kwamba kila mtu
ana mambo yake hakuna ukaribu kabisa lakini ndani ya chumba cha kubadilishia
nguo tuko pamoja. Cristiano sio diva."
Katika hatua
nyingine, Alonzo amesisitiza umuhimu wa nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno
katika kikosi cha Real Madrid na hakuna kingine isipokuwa maneno mazuri kwa
kocha Jose Mourinho.
"ni
mchezaji mwenye nia na mwenye kujiamini. Ni mchezaji muhimu katika timu"
"kila
siku najifunza kutoka kwa Mourinho. Ni mtu mwenye kutaka na anazingatia kila
kitu.
“watu
wanadhani wanamjua lakini naona wanamuangalia kwa muonekano wa nje. Namfahamu ndani
ya chumba cha kubadilishia nguo ni mtu tofauti sana.”
Ronaldinho kuingia mkataba mpya na Atletico
Mineiro.
Kiungo mbrazili
Ronaldinho Gaucho anajipanga kufanya mazungumzo ya kuingea upya mkataba na
klabu yake ya Atletico Mineiro wiki ijayo.
Kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 32 alikuwa akihusishwa na kutaka kuelekea katika vilabu
vya Fluminense na Santos baada ya kuonyesha kiwango safi jambo ambalo limepelekea
klabu yake kumtayarishia mkataba mwingine haraka haraka.
Wakala wa Ronaldinho
ambaye pia ni kaka yake Roberto Assis amerudia kauli yake kuwa atatoa taarifa
rasmi lakini kwasasa mpango huo uko
katika hatua za mwishoni.
Ronaldinho bado
ana matumaini ya kurejea katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil, na
kulikuwepo na tetesi kuwa uhakika wa kupata nafasi katika klabu yake ya Atletico
Mineiro ndiyo sababu kubwa inayo mfanya asiondoke katika klabu hiyo.
Joe Cole: Bado nitaendelea kuwepo Liverpool.
Joe Cole
anaamini kuwa bado ana nafasi ya kuendelea kuwepo Liverpool baada ya kuonyesha soka safi
katika mchezo dhidi ya Young Boys mchezo wa michuano ya ligi ya Ulaya.
Cole alifunga
goli moja na kusababisha lingine katika mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya
mabao 2-2 mchezo uliofanyika Anfield.
Cole mwenye
umri wa miaka 31 anasema alikuwa katika kiwango safi katika vilabu vingine kabla ya Liverpool na
amesisitiza kuwa anarejesha uwezo wake baada ya kufanikiwa kurejesha uimara wa
mwili wake kimazoezi na kuponya majeraha ya msuli.
“nilikuwa
mchezaji mzuri West Ham, Chelsea na Lille nadhani nitakuwa mchezaji mzuri Liverpool
pia,”
"ninaimarika
katika kila mchezo.
Ni kawaida mchezaji kutaka kucheza kila mchezo. Huu ulikuwa
mchezo wangu wa tatu kutoka katika maumivu ya msuli najisikia vizuri."
No comments:
Post a Comment