Mwasisi wa
kandanda la Cameroon Roger Milla ametaka kuwepo na utulivu baada ya taarifa
kuwa kiungo Alex Song alitupiwa maneno machafu na mashabiki wenye hasira nchini
kwake.
Hali hiyo
imekuja kufuatia Cameroon kuchapwa na Libya katika mchezo wa kuwania tiketi ya
kucheza kombe la dunia 2014.
Milla amesema
hayo alipokuwa akiongea na redio ya taifa.
Amewataka mashabiki
kuwa nyuma ya timu yao kuelekea kwemye mchezo wa kampeni ya kusaka tiketi
kucheza fainali ya mataifa ya Afrika dhidi ya Guinea Bissau mwishoni mwa juma
hili.
Kumbuka Cameroon
ilishinda katika mchezo wa kwanza kwa bao 1-0 mchezo ulipigwa mwezi February.
Soka la nchi
hiyo limekuwa katika hali tete baada ya Milla kuvuliwa uongozi wa heshima
katika shirikisho la soka la nchi hiyo kufuatia ukosoaji wake kwa wale wanao
liongoza soka nchini humo.
Hata baada
ya ya ushindi wa nyumbani dhidi ya DR Congo wa kampeni ya kufuzu kombe la dunia
2014 mashabiki wan chi hiyo walipandwa na hasira kiasi kutupa mawe katika basi
la wachezaji wakisema ushindi huo ulikuwa wa bahati.
Wachezaji sasa
hawapandi basi la timu ya taifa wakati wakisafiri nchini humo kwa tahadhari.
Taarifa za
mwanzo ziliarifu kuwa Song alivamiwa na mashabiki katika viunga vya Kennedy
Avenue mjini Yaounde lakini mchezaji
huyo alisema alichofanyiwa ni kuzungukwa na kutupiwa maneno ya jazba.
No comments:
Post a Comment