Mateo Musacchio |
Uongozi wa klabu ya Tottenham upo katika mazungumzo na
klabu ya Villarreal kwa ajili ya kutaka kukamilisha mpango wa kumsajili beki
kutoka nchini Argentina Mateo Musacchio.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewana kituo cha televisheni
cha SKY SPORTS cha nchini UIngereza, Tottenham wameanzisha mazungumzo hayo huku
wakiamini kiasi cha paund million 17 kitatosha kukamilisha usajili wa beki huyo
mwenye umri wa miaka 23.
Sifa kubwa ambayo inatumiwa na Spurs kwa kutaka kumsajili
Mateo Musacchio ni faida ya kucheza katika nafasi ya beki wa kati na pia
kucheza katika nafasi ya beki wa pembeni hivyo wanaamini endapo watamsajili
watakuwa wametimiza malengo ya kuziba nafasi mbili kwa mchezaji mmoja.
Mpaka sasa Mateo Musacchio tayari ameshaitumikia klabu yake
ya Villareal katika michezo 32, ambapo inaaminiwa ni kipimo kizuri kwake katika
harakati za kuhamishia uwezo wake kwenye ligi ya nchini Uingereza.
Meneja mpya wa klabu ya Tottenham Mauricio Pochettino,
tayari ameshakamilisha usajili wa wachezaji wanne ambao anaamini watakiboresha
kikosi hicho ambacho msimu uliopita kilikuwa chini ya meneja Tim Sherwoods.
Wachezaji waliosajiliwa na Spurs katika kipindi hiki ni Ben
Davies, Michel Vorm pamoja na Eric Dier huku beki wa kati kutoka nchini Ubelgiji
Jan Bert Lieve Vertonghen akihusishwa na taarifa za kutaka kuihama klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment