KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, August 5, 2014

KMKM ya Zanzibar kutua Kigali kesho kwa ajili ya michuano ya Kagame

Mabingwa wa soka visiwani Zanzibara KMKM kesho wanatarajia kuondoka visiwani ungunja kuelekea mjini Kigali nchini Rwanda tayari kwa ushiriki wa michuano ya kombe la Kagame ambayo imepangwa kuanza August 08.

Afisa habari wa KMKM Sheha Khamis amesema tayari maandalizi ya safari ya kikosi chao kuelekea mjini Kigali yameshakamilika, na kwa mwaka huu wamejipanga kusaka mafanikio zaidi kwa lengo la kufika kwenye mchezo wa hatua ya fainali.

Sheha amewataka watanzania wote kuwa kitu kimoja na kuwaombea dua wakati wote watakapokuwa mjini Kigali wakishiriki michuano hiyo, ili waweze kufanikisha lengo la kufanya vizuri.