Brendan Rogers atoa sababu za kufungwa na United katika International Champions Cup. |
Meneja wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers, ameelezea
hisia zake baada ya kupoteza mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya International
Champions Cup dhidi ya Man Utd uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo mjini Miami
nchini Marekani.
Rodgers, amesema matokeo ya mchezo huo hayajamvunja moyo wa
kuendelea kukiamini kikosi chake ambacho August 16 kitaanza mshike mshike wa
kusaka ubingwa wa nchini Uingereza, baada ya kukosa nafasi ya kutawazwa kuwa
mabingwa msimu uliopita.
Amesema kikosi chake hakikucheza vibaya katika mchezo huo
ambao ulihudhuriwa na mashabiki wengi, lakini makosa madogo madogo yaliwafanya
wachezaji wake kujikuta wakiadhibiwa na Man Utd kwa kufungwa mabao matatu kwa
moja.
Katika mchezo huo Liverpool walikuwa wa kwanza kupata bao
kwa njia ya mkwaju wa penati uliopigwa na kiungo na nahodha Steven Gerrard lakini
Man Utd waligeuka na kupata mabao matatu yaliyopachikwa wavuni na Wayne Rooney,
Juan Mata pamoja na Jesse Lingard.
Katika hatua nyingine meneja huyo kutoka Ireland ya
Kaskazini ameahidi kufanya usajili wa mchezaji mmoja ama wawili katika kipindi
hiki cha kuelekea mwanzoni mwa msimu wa ligi.
Wachezaji ambao wanadhaniwa huenda wakawa njiani kujiunga
na klabu hiyo ya Anfield ni beki wa kuliwa kutoka nchini Hispania na klabu ya
Atletico Madrid Javier Manquillo pamoja na Alberto Moreno PĂ©rez anaecheza
nafasi ya beki wa kushito kwenye klabu ya Sevilla.
Wakati huo huo, Rodgers amethibitisha kiungo mshambuliaji
kutoka nchini Brazil Philippe Coutinho, anakaribia kusaini mkataba mpya wa
kuendelea kuitumikia klabu ya Liverpool baada ya kuonyesha kiwango kizuri tangu
aliposajiliwa akitokea Inter Milan.
No comments:
Post a Comment