KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, June 14, 2012

Russia kukata rufaa EUFA


Russia’s football union imetangaza kuwa itakata rufaa juu ya adhabu waliyopewa na UEFA kufuatia tabia ambaya iliyoonyeshwa na mashabiki wa Russia katika mchezo dhidi ya Czech Republic ijumaa.
Adhabu iliyowekwa na UEFA ni penati ya kunyimwa points sita katika michezo ya kufuzu fainali za ulaya mwaka 2016 lakini endapo tu mashabiki wao watarudia tena kitendo hicho kwa vitendo vya vurugu ambavyo mashabiki walifanya huko Wroclaw. Adhabu nyingine ambayo imewakumba ni kupigwa faini ya euro €120,000.
Taarifa ya Football Union of Russia (RFS) imetolewa na kunukuliwa kupitia mtandao ikisema
“shirikisho la kandanda la Russian inaandaa na kuwasilisha rufaa dhidi ya maamuzi ya UEFA na hilo litafanyika ndani ya kipindi kilichowekwa kwa ajili ya taratibu hizo. Shisrikisho litafanya hivyo kuhakikisha timu ya taifa inaepuka adhabu hiyo”
Taarifa ya UEFA baada ya adhabu hiliyotolewa jumatano ilisema
 “bodi ya UEFA ya kudhibiti mwenendo wa nidhamu imeamua kuweka punguzo la points sita kwa shirikisho la soka la Russia RFS katika michezo ijayo ya kuwania kufuzu michuano ya.
Russia pia huenda ikakumbana na adhabu nyingine ya endapo UEFA itathibtisha kufuatia mlinzi wa Czech Theodor Gebre Selassie kutoa maelezo ya kufananishwa na nyani katika mchezo ambao timu hizo mbili zilipokutana katika mchezo wa ufunguzi.
Jumapili RFS ilitoa taarifa iliyoambatana na madai ya mchezaji huyo kuwa mashabiki walimfanyia dhihaka hiyo na EUFA inasema italitazama dai hilo kwa lengo la kupatia fidia kwa wale mashabiki wanao sababisha usumbufu kwa vitendo visivyokuwa vya kiungwana

No comments:

Post a Comment