KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, June 15, 2012

RAIS MSTAAFU ALHAJI ALI HASANI MWINYI AWAAMBI UKWELI VYAMA VYA MICHEZO.


Mfungaji wa bao la Taifa Stars dhidi ya Zambia mwaka 1979 bao la kufuzu fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika nchini nigeria Peter Tino tanzania(Picha kwa masaada wa Bin Zubeir blog) 
Rais mstaafu wa awamu ya pili wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi amewataka viongozi wa vyama vya michezo kufanya kwanza maandalizi kwa wanamichezo toka katika vyama vyao kabla ya kuelekea katika michuano mbalimbali wanayokabiliana nayo kuliko kulalamikia udhamini kwa wanamichezo wao kabla ya safari ya kuelelea katika michuano hiyo.
Kauli hiyo ameitoa wakati hafla ya utoaji tuzo za wanamichezo bora wa mwaka 2011 zilitolewa na chama cha waandishi wa habari za michezo nchini Tanzania taswa.
Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Diamond jubilee jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanamichezo wa kada tofauti, waandishi wa habari na wageni wengine mbalimbali waalikwa.
Alhaji mwinyi amesema si vema viongozi wa michezo kulalamikia kukosa udhamini wakati ambapo wachezaji wamekosa maandalizi na mara baada ya kupata udhamini huo matokeo yake ni kushindwa vema na kurejea nyumbani kwa madai ya maandalizi hayakuwa mazuri huku akitumia msemo wa “aibu yao ni aibu yetu”
Alhaji mwinyi amevitaka pia vyama vya michezo kuanza mchakato wa kusaka vipaji vya vijana kuanzia umri mdogo na kutengeneza hazina kubwa katika vyama vyao na kuachana na zama za kichwa cha mwendawazimu.
Katika tuzo hizo mcheza soka wa klabu ya Simba Shomari Kapombe alitajwa kuwa mwanamichezo bora wa mwaka 2011 tuzo ambayo imeambatana na zawadi ya pesa taslimu shillingi milioni kumi na mbili.
Pamoja na tuzo hiyo Kapombe alitajwa kama mchezaji bora chipukizi.
Alhaji Ali Hassani Mwinyi akimkabidhi Shomari Kpombe hundi ya pesa ya milioni kumi na mbili  ya mchezaji bora wa mwaka wa TASWA mwaka 2011(picha kwa msaada wa Bin Zubeir)
Wachezaji wengine walioshinda tuzo katika hafla hiyo ni Emmanuel Okwi wa Simba ambaye ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa nje ya nchi, Mbwana Samatta wa TP Mazembe ya DRC kama mchezaji bora wa Tanzania anayecheza soka nje ya nchi pamoja , Aggrey Morris wa Azam kama mchezaji bora wa kiume na Mwanahamisi Omari akishinda tuzo ya mchezaji bora wa soka la wanawake.

Orodha kamili ya tuzo za chama cha waandishi wa habari Tanzania(TASWA) ni kama ifuatavyo

1: OLIMPIKI MAALUM-Zanzibar
Ahmada Bakar:
 2:OLIMPIKI MAALUM-TANZANIA BARA
HERITH SULEIMAN
 3: PARALIMPIKI: WANAUME
ZAHARANI MWENEMTI
4:PARALIMPIKI: WANAWAKE
FAUDHIA CHAFUMBWE
5: KIKAPU: WANAUME
GEORGE TARIMO:
6:  KIKAPU WANAWAKE
EVODIA  KAZINJA:-
 7: NETIBOLI:
LILIAN SYLIDION
 8:  GOFU WANAWAKE:
MADINA IDDI
9: GOFU WANAUME:
Frank Roman:
10: NGUMI ZA RIDHAA
SULEIMAN SALUM KIDUNDA
 12:  WAOGELEAJI MWANAMKE
MAGDALENA MOSHI     
 WAOGELEAJI MWANAUME
AMMAAR GHADIYALI  -  MEN
13:JUDO...
AZZAN HUSSEIN KHAMIS (ZANZIBAR)
14:JUDO BARA: . MBAROUK SELEMANI
 14: WAVU WANAWAKE
THERESIA ABWAO  
15: WAVU WANAUME
MBWANA ALLY
16: NGUMI ZA KULIPWA
 Nasibu Ramadhan
 17. TENISI:Wanaume
WAZIRI SALUMU
 18. TENISI WANAWAKE: 
REHEMA ATHUMANI

20: BAISKELI (Wanawake)
Sophia Hussein
21: BAISKELI WANAUME
Richard Laizer
22: WACHEZAJI WA TANZANIA WANAOCHEZA NJE
Mbwana Samatta-
 23: MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI
SHOMARI KAPOMBE- (soka) SIMBA
24: MCHEZAJI WA NJE ANAYECHEZA TANZANIA
Emmanuel Okwi-Simba
25: SOKA (WANAWAKE)
MWANAHAMISI OMARI
 26: SOKA WANAUME
Aggrey Morris-Azam:
27: RIADHA
WANAWAKE
Zakia Mrisho:
28: RIADHA WANAUME
Alphonce Felix:
 29: MIKONO WANAUME
Kazad Monga-Magereza Kiwira
Faraji Shaibu  Khamis-Nyuki Zbar
 30:  MIKONO WANAWAKE
Zakia Seif-Ngome Dar
31: Kriketi WANAWAKE
Miss. Monika Pascal
32; KRIKETI WANAUME
Mr. Kassimu Nassoro
 33: TUZO YA HESHIMA:
KIKOSI KILICHOFUZU FAINALI ZA MATAIFA YA AFRIKA 1980
34:MWANAMICHEZO BORA WA TANZANIA MWAKA 2011-
SHOMARI KAPOMBE 

Shomari Kapombe akipokea tuzo ya mchezaji bora chipukizi

Aggrey Morris akipokea tuzo ya mchezaji bora wa soka wa mwaka 2011

 Katika utoaji wa tuzo hizo za mwaka huu taswa imewakumbuka wachezaji wote waliokuwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania (TAIFA STARS) walioshiriki fainali ya mataifa ya Afrika mwaka 1980 Lagos nigeria kwa kuwapa tuzo ya heshima ambapo wachezaji wote walio hai wamealikwa na kuhudhuria wakiongozwa na aliyekuwa mlinzi wa kati na nahodha wa kikosi wakati huo ambaye kwasasa ndiye Rais wa shirikisho la soka nchini Tanzania Leordigar Chila Tenga.
wengine waliohudhuria mbali na Tenga ni Daudi Salum, Adolf Rishard,Peter Tino, Shabani Ramadhani, Leopard Taso Mukebezi, Omari Hussein, Omari Kapenta, Juma Mkambi, Omary Mahadhi,Hussein Ngulungu, Jellah Mtagwa, Shabani Katwila na Juma Pondamali"Mennsah"

hawa ni baadhi ya wachezaji wa zamani waliokuwepo katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania cha mwaka 1980 nchini Nigeria kutoka kushoto ni Adolf Rishard, Daudi Salum ,Leodiger Tenga, Jellah Mtagwa wakimsikiliza kwa makini rais mstaafu wa awamu ya pili alhaji Ali Hassan Mwinyi.
(Picha kwa msaada wa Bin Zubeir)