Van Persie mchezaji bora wa mwezi disemba
wa Premier League.
Mshambuliaji
wa Manchester United Robin van Persie ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwezi
disemba wa ligi kuu ya nchini England ‘Premier League’.
Mdachi huyo
amefunga mara tano katika michezo sita aliyoicheza timu ya mashetani wekundu
katika cha mwezi huo ambapo ameiwezesha timu hiyo kutengenezwa mwanya wa alama
saba ndani mwezi huo ambayo ulikuwa na ratiba ya michezo ya sikukuu za
Chrismass na mwaka mpya.
Van Persie, ambaye
kwasasa anaongoza katika chati ya ufungaji magoli akiwa na magoli 16 ametanabaisha
kuwa anafurahia kupata tuzo hiyo ya mwezi kutoka kwa wadhamini Barclays.
Van Persie alijiunga
na United akitokea Arsenal kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 24 million katika
uhamisho wa kipindi cha majira ya kiangazi na tangu wakati amekuwa kicheza
katika michuano yote na ameshatia kambani jumla ya magoli 20.
Shakhtar yaizidi kete Chelsea yamsajili
Taison wa Metalist.
Shakhtar
Donetsk imethibtisha kumsajili Taison toka klabu ya Metalist Kharkiv kwa ada ya
euro milioni 15 ambapo mchezaji huyo raia wa Brazilian amenguka saini ya
mkataba wa miaka mitano.
Taarifa ya
klabu hiyo imesema
"Januari
10, Rais wa Shakhtar na Metalist walikuwa na mazungumzo juu ya uhamisho wa Taison
kutoka mji wa Kharkiv kuelekea mji mwingine wa Donetsk, Shakhtar imelipa dolari
za kimarekani milioni 20 na kwamba tumepata mchezaji ambaye alikuwa anataka
kujiunga nasi tumempa mkataba wa miaka 5 "
Mshambuliaji
huyo alijiunga na Metalist akitokea Internacional mwaka 2010, na ameitumikia
klabu hiyo kwa michezo 57 ambapo alifunga jumla ya magoli 13 goals.
No comments:
Post a Comment