Deogratius Lyato. |
SHIRIKISHO la soka nchini TFF limetangaza rasmi kuwa tarehe ya uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo ni 24/02/2013 ambapo uchaguzi huo utafanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF Degratius Lyato amesema fomu za kuwania nafasi ya urais, makamu wa Rais na ujumbe wa kamati ya utendaji zitaanza kutolewa Januari 14 ambapo zoezi hilo litaendelea mpaka Januari 18 katika ofisi ya katibu mkuu wa shirikisho hilo na idara ya uhasibu kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 10 jioni.
Amesema kwa nafasi ya mwenyekiti fomu hizo zitauzwa kwa shilingi laki 5, makamu wa Rais shilingi milioni 2 wakati ambapo kwa nafasi ya ujumbe fomu hizo zitauzwa kwa shilingi laki 2.
Mbali na hilo pia kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa bodi ya inayosimamia ligi uchaguzi ambao utafanyika februari 22 ambapo fomu kwa upande huo zitaanza kutolewa januari 14 mpaka 18.
Amesema nafasi zinazogombewa ni mwenyekiti wa bodi na makamu mwenyekiti ambapo ada ni shilingi laki 2.
Amesema kwa wale wanaotaka nafasi ya kamati ya uongozi ada itakuwa ni shilingi laki moja.
Pia Lyato amesema kwa mujibu marekebisho ya katiba ni kwamba mwenyekiti na makamu wa mwenyekiti bodi hiyo watakuwa moja kwa moja ni wajumbe wa kamati ya utendaji ya TFF na kwamba chaguzi zote zitafanyika jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment