Vigogo vya soka barani barani Ulaya vimekaribia kukata tiketi za kucheza fainali ya kombe
la dunia nchini Brazil wakati ambapo kutoka barani Afrika Ghana imefanikiwa kutika katika kundi la timu10 za mwisho zitakazo cheza hatua ya mtono kabla ya kufuzu kuingia katika fainali za kombe la dunia mwakani
nchini Brazil.
Uhispania , Ujerumani na Italia zimesogea ukingoni mwa kufuzu kukata
tiketi ya fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil huku Cristiano
Ronaldo akipachika mabao matatu ya haraka na kuiweka Ureno katika njia
ya kuelekea Brazil pale Ureno ilipokuwa ikipambana na Ireland ya kaskazini.
Safari ya Uholanzi kuelekea katika fainali hizo zitakazofanyika mwakani
majira ya joto huko Brazil ilipunguzwa kasi mara baada ya kwenda sare dhidi ya timu
dhaifu ya Estonia ilhali Uingereza ikipanda juu ya msimamo wa kundi lake
kwa ushindi wa kishindo wa mabao 4-0 dhidi ya Moldova.
Ujerumani haikufanya mzaha kabisa hiyo jana dhidi ya majirani zao Austria
ikiwa katika azma yao ya kuelekea nchini Brazil mwakani baada ya kuinyoa bila
maji kwa mabao 3-0.
.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa ukibadilika badilika, kikosi cha kocha
Joachim Loew kiliwabana vilivyo wadogo zao hao wa Austria na
kujisafishia njia kuelekea Brazil mwakani.
Matukio matatu muhimu ya
kukumbukwa yalitokea katika mchezo huo wa jana ambapo mshambuliaji
Mroslav Klose amepachika hatimaye bao lake ya 68 akitimiza mabao sawa na
mshambuliaji hatari wa Ujerumani , Gerd Mueller ambaye katika enzi zake
alipachika mabao 68 katika timu ya taifa.
Nahodha wa kikosi cha Ujerumani Philip Lam ameiongoza timu hiyo jana
akicheza kwa mara ya 100 katika jezi ya Ujerumani na nahodha wa zamani
Michael Balack ameagwa rasmi akiwa katika jezi ya Ujerumani katika mchezo huo akiwa katika benchi.
Amenukuliwa nahodha Philip Lam akisema
."Kulikuwa na sababu ya kufurahi kwa kikosi kizima cha Joachim Loew kwa
kuwa mara kadha Austria imekuwa kikwazo kikubwa kwa Ujerumani katika
michezo kama hiyo"
.
"Katika mchezo ambao timu unayopambana nayo iko nafasi ya pili katika
kundi letu kushinda mabao 3-0 nyumbani ni kitu kizuri sana. Tumeshinda
kwa sababu tulifanya juhudi kubwa na hatukutoa nafasi kwa adui kufanya
mashambulizi ya hatari, na upande wa mbele tulikuwa wabunifu na
tulicheza kama tulivyoelekezwa kufanya".
Ni furaha kubwa
Mshambuliaji wa pembeni Thomas Müller ambaye alipachika mabao matatu katika mchezo huo na kutengeneza la kwanza ambalo liliwekwa wavuni na
Miroslav Klose amesema anajisikia vizuri kuwamo katika kikosi hicho cha
DFB.
Nahodha wa Ujerumani wa sasa Lam kati na nahodha wa zamani Michael Bakack (aliyeshika maua)wakipewa tuzo.
"Najisikia vizuri sana , kwamba niliweza kusaidia mabao mawili. Goli la
Toni lilikuwa muhimu na kiufundi lilikuwa bao safi kabisa".
"Na tulikuwa
na wakati ambapo hatukuweza kuwa makini kupeleka mpira mbele , kwa kuwa
haiwezekani kupeleka mpira kuelekea goli la adui kwa muda wote wa dakika
90 kwa kuwa sisi ni binadamu" .
"Lakini , baada ya mabao 3 , Austria
haikuwa na fursa ya wazi ya kupata bao. Hatukuwapa nafasi hiyo , kwa
jumla tumeridhika".
Sweden inaendelea kuwa mpinzani hatari anayeifuatia Ujerumani katika
kundi C .
Sweden ilikishinda kikosi cha Ireland cha kocha mkongwe
Giovani Trapatoni kwa mabao 2-1. Licha ya kuwa kocha huyo mkongwe
anamatumaini bado kuwa kikosi chake kinaweza kukata tiketi kwenda Brazil
licha ya matokeo hayo ya kukatisha tamaa.
Kocha huyo raia wa Italia
amesisitiza kuwa kikosi chake kinahitaji points 4 kutoka mechi mbili.
wapinzani wao katika mchezo unaofuata Jumanne ijayo ni Austria na baada
ya hapo kikosi hicho cha Trapatoni kinakwaana na Ujerumani.
Katika usiku uliokuwa na heka heka nyingi , Ubelgiji imerefusha uongozi
wake katika kundi A hadi points 5 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya
Scotland, Bosnia Herzegovina iliteleza nyumbani dhidi ya Slovakia kwa
kuchapwa bao 1-0 , wakati Ugiriki ilikuwa mshindi dhidi ya Liechtenstein
na kufungana kileleni mwa kundi G.
Ghasia zimechafua ushindi wa mabo 3-0 wa Romania dhidi ya Hungary na
Ukraine imepata ushindi mnono wa mabao 9-0 dhidi ya San Marino katika
kundi H.
Montenegro ilipoteza kiti chake cha uongozi katika kundi hilo
baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Poland na unashikilia usukani
pamoja na Uingereza zikiwa zote na points sawa.
Italia imesogea karibu na kukata tikiti yake kwenda Brazil baada ya
ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Bulgaria, wakati jamhuri ya Czech
imepigwa butwaa baada ya kusalim amri kwa kufungwa mabao 2-1 nyumbani
dhidi ya Armenia.
Hodgson ashindwa ampange nani
Kocha wa Uingereza Roy Hodgson amekiri kuwa yuko katika hali ya
kuchanganyikiwa kidogo baada ya kocha huyo wa Uingereza kushindwa
kufanya uchaguzi katika sehemu ya ushambuliaji licha ya ushindi wa mabao
4-0 dhidi ya Moldova jana.
Mshambuliaji wa Manchester United Danny Welberk , alionyeshwa kadi ya
njano jana ambayo inamzuwia kucheza katika mchezo dhidi ya Ukraine
Jumanne ijayo , timu ambayo iko nyuma ya Uingereza kwa points moja tu.
Wayne Rooney na Andy Carroll hawatacheza kwa sababu ni majeruhi na
Daniel Sturridge huenda akashindwa kucheza kwa kuwa ana maumivu ya paja,
hali hiyo inamuacha Hodgson na chaguo la Rickie Lambert ama Jermain
Defoe ambao ndio washambuliaji wake ambao wako fit.
Cristiano Ronaldo ameiokoa Ureno kwa kupachika mabao matatu ya haraka
haraka na kuipa timu yake sare muhimu dhidi ya Ireland ya kaskazini,
wakati Uholanzi imepoteza points mbili za kwanza katika kinyang'anyiro
hiki cha kuwania kufuzu kwenda Brazil kwa kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi
ya Estonia.
Lakini Ronaldo hatakuwamo katika kikosi hicho wakati kikatakapocheza
mchezo wa kirafiki Jumanne ijayo dhidi ya Brazil mjini Boston kutokana
na maumivu.
Ghana yajaribu bahati
Katika bara la Afrika kikosi cha Black Stars ya Ghana , imenyakua moja
kati ya nafasi saba zilizobaki katika kinyang'anyiro cha kufuzu kucheza
katika fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil katika kanda ya
Afrika , wakati timu hiyo iliyofikia robo fainali mwaka 2010 ikiishinda
Zambia kwa mabao 2-1 katika kundi la D.
Zambia mabingwa wa mataifa ya Afrika mwaka 2012 imeondolewa katika
kinyang'anyiro hicho cha kuwania nafasi ya kucheza katika fainali za
kombe la dunia.
Wakati Michael Essien akirejea katika kikosi hicho baada ya kukaa nje
kwa muda mrefu kutokana na mauamivu, ushindi wa Ghana katika uwanja wa
Baba Yara mjini Kumasi unaifanya timu hiyo kujiunga na Cote D'ivoire,
Misri na Algeria katika michezo ya mchujo mwezi Oktoba na novemba mwaka
huu na kuamua ni timu gani itaingia katika kundi la timu tano kutoka
bara la Afrika kucheza kule Brazil mwakani.
Timu nyingine sita zitakazojiunga na timu hizo zitaamuliwa
leo(07.09.2013) na kesho Jumapili(08.09.2013). Baadhi ya vigogo vya soka
la Afrika , Nigeria , Cameroon, Senegal na Tunisia ni miongoni mwa timu
ambazo zitaweza kujiwekea nafasi katika michuano hiyo itakayofanyika
nyumbani na ugenini.
Argentina na Colombia hazijaweza kukata tikiti zao jana huenda hadi
mchezo ujao baada ya uruguay kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Peru
jana.
Chile iliishinda Venezuela kwa mabao 3-0 na kupanda juu hadi nafasi ya
tatu katika msimamo wa kundi la America ya kusini, points mbili nyuma ya
timu hizo mbili za juu.
Wakati kinyang'anyiro hicho kinachoshirikisha timu 16 kitakapomalizika
mwezi ujao , timu nne za juu zitakuwa zimekata tikiti zao kwenda Brazil
mwakani wakati timu itakayomaliza nafasi ya tano itapambana na ama
Jordan ama Uzbekistan mwezi Novemba ili kupata nafasi moja iliyo wazi.
Kocha aliyeitawaza Bayern Munich kuwa mabingwa wa champions league msimu
uliopita , mabingwa wa Bundesliga na kombe la shirikisho DFB Pokal
nchini Ujerumani msimu uliopita, Jupp Heynckes ametunukiwa medali ya
Fairplay ya shirikisho la soka la Ujerumani, DFB kwa kukiongoza kikosi
hicho cha Super Bayern kupata mataji matatu katika msimu mmoja.
Tennis.
Bingwa mtetezi Serena Williams aliingia katika fainali ya mchezo wa
tennis ya US Open akipambana na Victoria Azarenka wakati wachezaji hao
wa juu wakipata ushindi katika michezo yao ya nusu fainali jana. fainali
hiyo itakuwa ni marudio ya fainali ambapo wasichana hao walipambana
tena katika fainali kama hiyo mwaka uliopita.
Riadha.
Usain Bolt yuko tayari sasa kwenda mapunzikoni baada ya kupata medali
nyingine tatu za dhahabu katika msimu mmoja ambapo alishindwa mara moja
tu , na hiyo ilikuwa kwa sekunde kiduchu tu.
Mjamaica huyo alishinda mbio za mita 100 kwa kutumia sekunde 9.80 katika
ligi ya diamond jana Ijumaa. Mchezaji mwenzake wa Jamaiya Asafa Powell
na Tyson Gay wa Marekani waligunduiliwa kuwa wanatumia madawa ya
kuongeza nguvu , na kuumia kwa hasimu wake mkubwa kutoka Jamaica Yohan
Blake kumewanyima wapenzi wa riadha washindani wao nyota katika riadha.
Mkutano wa kamati ya IOC
Kamati ya kimataifa ya olimpiki IOC, imeanza rasmi kikao chake muhimu za
maamuzi jana Ijumaa(06.09.2013) mjini Buenos Aires. Wajumbe wa kamati
hiyo wanakabiliwa na majukumu matatu muhimu hadi siku ya Jumanne.
Leo Jumamosi(07.09.2013) wanakabiliwa na uteuzi wa mji mwenyeji wa
mashindano ya michezo ya olimpiki ya mwaka 2020 baina ya Tokyo, Istanbul
na Madrid. Baadaye wanapaswa kuteua mchezo mmoja katika michezo ya
olimpiki , ama mchezo wa Squash, mieleka ama softball ama baseball, na
siku ya Jumanne wajumbe watachagua mrithi wa rais wa IOC Jacques Rogge
kutoka orodha ya wagombea sita.
No comments:
Post a Comment