Mart Noij kocha wa Stars |
Wakati Taifa Stars inaingia kambini Tukuyu mkoani
Mbeya kesho (Julai 9 mwaka huu), kocha Martinus
Ignatius 'Mart Nooij' amesema kambi ya wiki mbili
nchini Botswana imekisaidia kikosi chake kujiandaa kwa ajili ya mechi dhidi ya
Msumbiji.
Mart Nooij amesema kikosi chake kipo vizuri kuelekea katika
mchezo wa kwanza wa hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kupangwa kwenye
makundi ya kuwania tiketi ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani
nchini Morocco dhidi ya timu ya taifa ya Msumbiji.
Nooij ametangaza uhakika huo hii leo mbele ya waandishi wa
habari ambapo amesema utayari wa kikosi chake kuikabili Msumbiji umekuja
kufutia maandalizi mazuri waliyofanya mjini Gaborone nchini Botswana kwa muda
wa majuma mawili.
Amesema kesho watakuwa wakielekea mjini Tukuyu mkoani
Mbeya kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya mchezo huo ambao umepangwa
kufanyika Julai 20 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Akizungumzia safari yake ya nchini Msumbiji ambayo
aliifanya kabla ya kuelekea Botswana nooij amesema hakwenda mjini Maputo kwa
kusudio la kuwachunguza wapinzani wake The Mambas balia likwenda kukamilisha
shughuli zake binafsi za kimaisha.
Hata hivyo kocha huyo kutoka nchini Uholanzi amekataa kata
kata kutoa ahadi kwa mashabiki wa soka nchini kuelekea katika mchezo huo dhidi
ya Msumbiji kwa kusema sio desturi yake kuahidi matokeo ili hali mchezo husika
ukiwa bado haujachezwa.
Kwa msisitizo zaidi Mart Nooij akatumia mfano wa mchezo wa
tennis kwa kusema mashabiki wa mschezo huo huwa hawaamini kama washiriki
wanaweza kushinda michezo yote, halia mbayo anaichukulia na kwake kama kocha wa
Taifa Stars.
Lakini pamoja na kusisitiza itikadi hiyo, Nooij amesema
bado ataendelea kutumia mfumo wa uchezaji kama alivyofanya wakati wa mchezo
dhidi ya Zimbabwe ambapo kikosi chake kilionekana kutumia nafasi pale ilipo
patikana.
Kitaalamu amesema kambi ya Tukuyu kama
ilivyokuwa ya Botswana itawasaidia kwa mechi dhidi ya Msumbiji.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium
Lager itaondoka kwa ndege kwenda Mbeya ikiwa na kikosi cha wachezaji 25, na
itarejea jijini Dar es Salaam siku tatu kabla ya mechi hiyo.
Wachezaji walioko kwenye msafara huo ni Aggrey Morris,
Aishi Manula, Amri Kiemba, Benedictor Tinoko, Deogratius Munishi, Edward
Charles, Emmanuel Namwando, Erasto Nyoni, Haruni Chanongo, Himid Mao, John
Bocco na Jonas Mkude.
Wengine ni Joram Mgeveke, Kelvin Friday, Kelvin
Yondani, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa, Mwagane Yeya, Nadir Haroub, Oscar Joshua, Pato
Ngonyani, Ramadhan Singano, Said Juma, Said Moradi, Shomari Kapombe na Simon
Msuva.
Mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya
kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Afrika (AFCON) dhidi ya Msumbiji
itafanyika Julai 20 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment