KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 8, 2014

Nahodha wa Stars 'Canavaro' awahakikishia watanzania kuwaondosha Msumbiji mashindano Afrika

Kikosi cha Taifa Stars kinaelekea kambini Tukuyu kabla ya kumsulubu Mamba wa msumbiji
Nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Nadir Haroub Ally 'Canavaro' amewataka wachezaji wenzake wa kikosi hicho kupambana vilivyo katika mchezo wao dhidi ya timu ya taifa ya Msumbiji maarufu kama Mamba ambao ni mchezo pekee uliosalia wa hatua ya mtoano kuwania kufuzu hatua ya makundi ya fainali za mataifa ya Afrika.

Canavaro amesema huo ni mchezo wa kufia uwanjani kwa kuwa endapo wataondolewa na majirani hao wa Tanzania kwa upande wa kusini mwa nchi,  wazi kuwa Stars haitakuwa tena na michezo mingine ya kimashindano kwa mwaka huu.

Akiwa ameambatana na mlinda mlango namba moja wa Stars Deogratius Munish 'Dida' katika mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa na kocha wa Stars Mart Noij, Canavaro amesema ni dhahiri kuwa kila mtanzania angependelea kuona wakipata matokeo mazuri jambo ambalo ni salamu tosha kwa wachezaji wenzake wa kikosi hicho ambao kisingi wanadhamana kubwa ya taifa hili katika mchezo huo.

Amesema kambi ya kikosi hicho nchini Botswana ilikuwa nzuri licha ya matokeo ya kufungwa michezo miwili ukiwemo mchezo dhidi ya wenyeji Botswana mara mbili 4-2, 2-1 na mchezo wa ushindi wa mabao 3-1. Amesema kikosi cha Botswana kilikuwa na wachezaji wengi wenye uzoefu wa nje ya nchi ukilinganisha na Tanzania ambayo karibu kikosi kizima kina wachezaji wa ndani ya nchi.

Canavaro amejinasibu ya kuwa yeye ni mpambanaji na kwamba atawashawishi wachezaji wenzake kuhakikisha wanatoka na ushindi katika mchezo huo unaotarajiwa kufanyika Julai 20 2014 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.