Manchester City, imethibitisha kumsajili golikipa Willy Caballero |
Klabu bingwa nchini Uingereza Man City, imekamilisha dili
la usajili wa mlinda mlango kutoka nchini Argentina, Willy Caballero akitokea
kwenye klabu ya Malaga ya nchini Hispania kwa ada ya uhamisho wa paund million 6.5.
Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 32, amekwenda
Etihad Stadium kwa urahisi, kufuatia mahusiano mazuri yaliopo kati ya viongozi
wa Malaga pamoja na meneja wa Man city, Mannuel Pellgrini.
Dhumuni kubwa la Pellegrini la kumsajili Caballero ni
kutaka kumpa changamoto mlinda mlango Joe Hart, ambaye ni chaguo lake la kwanza
kuhakikisha anatunza uwezo wake katika kipindi chote cha msimu ujao, la sivyo
huenda akaipoteza nafasi hiyo.
Dakika kadhaa baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na
Man City, Caballero amezungumza na kituo cha televisheni cha klabu hiyo na
kuelezea furaha yake ambapo amesema ni faraja iliyoje kwake kujiunga na klabu
kubwa tena yenye sifa mjini Manchester na kwingineko.
“Ujio wangu Man City natambua ni mtihani kwangu pamoja na
Joe Hart, itanilazimu kucheza kwa kujituma wakati wote kwa ajili ya kutimiza
malengo yangu na ya klabu pia.” Amesema Willy Caballero
“Nafahamu Joe Hart ni
mlinda mlango mzuri, tena mwenye viwango vya hali ya juu, lakini ujio wangu
haumaanishi kama nimekuja hapa nishindane naye, ila nina uhakika kila mmoja
atapewa nafasi kutokana na uwezo wake wa kuisaidia klabu ya Man city yenye
lengo la kutaka kutetea ubingwa wa Uingereza msimu ujao.” Amesisitiza Caballero.
Kusidio lingine la kusajiliwa kwa Willy Caballero huko
Etihad Stadium ni kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mlinda mlango kutoka nchini
Romania Costel Fane Pantilimon, ambaye ametimkia kwenye klabu ya Sunderland
kufuatia mkataba wake kumalizika.
No comments:
Post a Comment