Wakala wa mshambulizi matata wa
Liverpool, Luis Suarez, amefanya mazungumzo na kocha wa klabu hiyo
Brendan Rodgers na mkurugenzi mkuu Iyan Ayre na kukariri kuwa mchezaji huyo kutoka Uruguay,
angali ana nia kubwa ya kushiriki katika michuano ya kuwania kombe la
klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao.
Pere Guardiola alisafiri hadi uwanja wa
Mesrseyside na kufanya mazungumzo na wawili hao, baada ya Liverpool
kusisitiza msimamo wao wa awali kuwa hawana nia ya kumuuza mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka ishirini na sita.
Suarez,
kwa sasa yuko likizoni, baada ya kuichezea timu ya taifa ya Uruguay,
wakati wa michuano ya kuwania kombe la Shirikisho nchini Brazil.
Lakini katika miezi ya hivi karibu, Suarez
amedokeza kuwa nia yake kuu msimu ujao ni kushiriki katika michauno ya
Ulaya na inaaminika kuwa wakala wake Pere Guardiola alisasilisha ujumbe
huo kwa wasimamizi wa klabuhiyo ya Liverpool hiyo jana.
Je ndoto ya Suarez itatimia?
Tayari Liverpool, imekataa ombi kutoka kwa klabu
ya Arsenal ya kutaka kumsajili mchezaji huyo kwa kitita cha pauni
milioni thelathini, licha ya kuwa mchezaji huyo ameelezea wazi wazi
kutoridhishwa kwake na maisha ya Uingereza.
Kocha wa Liverpool Brenda Rogers vile vile ameshikilia uzi huo huo wa bodi ya wakurugezi kuwa Suarez haendi kokote.
Suarez anatumikia adhabu ya kutoshiriki katika mechi kumi baada ya kupatikana na hatia ya Branislav Ivanovic wakati wa
mechi yao katika uwanja wa Anfeld msimu uliopita na katika siku za hivi
karibuni amekuwa akihusishwa na klabu ya Real Madrid.
Ripoti zinasema huenda Liverpool, ikakubali ombi
kutoka kwa klabu ambayo itakuwa tayari kulipia takriban pauni milioni
hamsini, sawa na kiasi ambacho Chelsea kililipa wakati ilipomsajili
Fernando Torres Janauri mwaka wa 2011.
Msimu uliopita, Suarez alishutumiwa sana,
kutokana na kile wakosoaji wake walitaja kuwa mtindo wa kujiangusha ili
kupata mkwaju wa adhabu
No comments:
Post a Comment