Paolo Di
Canio amekanusha kuwa matembezi yake yakutembelea uwanja wa Madejski mwishoni
mwa wiki kuwa kuna uhusiano na kuondoka kwa aliyekuwa meneja wa Reading Brian
McDermott.
Bosi huyo wa
zamani wa Swindon alipigwa picha akiwa katika eneo la wakurugenzi wa klabu ya
wakati wa mchezo ambao Reading walifungwa kwa mabao 2-1 na Aston Villa.
Kuonekana kwake
katika mchezo huo kulichukuliwa kama ni sehemu ya mchakato wa kuelekea kuchukua
nafasi ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo aliyetupiwa virago vyake McDermott.
Di Canio amekaririwa
na BBC Sport Di Canio akisema kuwa alikwenda katika mchezi huo kwa lengo ka
kuangalia mchezo huo na si vinginevyo.
McDermott meneja
wa zamani wa Reading alifukuzwa kazi na Reading Jumanne wiki hii baada ya
kupata matokeo mabaya ya kufungwa michezo minne mfululizo ya ligi kuu ya soka
nchini England.
Droo ya robo
fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya imefanyika hii leo ambapo mabingwa mara nne
wa taji hilo Barcelona watakuwa wakocheza dhidi ya vinara wa ligi kuu nchini
Ufaransa Paris Saint-Germain.
Michezo ya mkondo
wa kwanza ya hatua hiyo ya robo fainali inatarajiwa kuchezwa April 2 na 3 kabla
ya michezo ya marudiano ambayo itachezwa April 9 na 10.
Kikosi cha Joes
Mourinho, Real Madrid chenyewe kitakuwa na kazi dhidi ya timu ya mshambuliaji wa
kimataifa wa Ivory Coast Didier Drogba, Galatasaray, wakati ambapo Bayern
Munich waliotinga fainali ya msimu uliopita wakikutana dhidi ya Juventus nao Malaga
dhidi ya Borussia Dortmund.
Droo hiyo
kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1996 itakuwa imezikosa timu za nchini England
katika hatua hiyo ya michuano.
Paris
Saint-Germain itakuwa na nahodha wa zamani wa England David Beckham ambaye
atakuwa akionekana katika hatua hiyo ya michuano ya vilabu Ulaya kwa mara ya
kwanza tangu mwaka 1995.
Meneja wa
zamani wa Chelsea Jose Mourinho atakuwa na kazi ya kusaka mbinu ya kulinda
makali ya mshambuliaji wake wa zamani katika klabu ya Chelsea Didier Drogba wakati
kigogo cha Hispania, Real Madrid watakapo kutana dhidi ya klabu mpya ya Drogba, Galatasaray.
Bayern
Munich ambao walipoteza katika fainali ya msimu uliopita kwa Chelsea watakuwa
na kazi dhidi ya Juventus ambayo
haijapoteza michezo yake ya msimu huu katika michuano hii.
Timu
nyingine ambayo haijapoteza mpaka sasa ni Borussia Dortmund ambao ambao watasafiri
nchini Hispania kuwafuata Malaga katika mchezo wa mkondo wa kwanza mchezo ambao
utakuwa ni kwanza kuwakutanisha katika michuano ya Ulaya.
No comments:
Post a Comment