Walinzi hawa sita wangeweza kusajiliwa na Arsenal kwani wamekuwa wakihama vilabu mbalimbali kwa gharama ndogo ambayo washika mitutu wanaweza kumudu. |
Mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakichangia kati ya pauni milioni £45 mpaka £90 kwa mwaka kupitia mapato ya tiketi kiasi ambacho kingewezesha meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger akisajili wachezaji sita wa eneo la ulinzi wa kati.
Washika mitutu wamekuwa katika shida katika eneo lao la ulinzi tangu kuanza kwa msimu ambapo nahodha wa zamani Thomas Vermaelen aliondoka na kujunga na Barcelona
bila ya pengo lake kuzibwa na mzee Wenger.
Sera za usajili za Wenger ni tatizo |
Majeruhi Mathieu Debuchy na Nacho Monreal, pamoja na kuugua kwa Calum Chambers, kumemlazimisha Wenger kumtumia nyota anayechipukia Hector
Bellerin katika roho ya ulinzi wa kikosi mchezo wa ligi ya mabingwa Borussia Dortmund mwezi uliopita.
Uchunguzi unaonyesha kuwa kiasi cha fedha ambacho mashabiki wanalipia katika kununua tiketi za msimu za washika mitutu hao kinaweza kuwa ni pungufu ya kiasi hicho cha fedha lakini swali ni vipi klabu hiyo imeshindwa kuimarisha ulinzi.
Bei ya chini ya tiketi katika uwanja wa Emirates ni pauni £1,014 ambapo bei ya tiketi ya gharama ni £2,013.
Hii ina maana kuwa kiwango cha chini kila mwaka kwa mauzo ya tiketi ni pauni milioni £45 kiasi ambacho Arsenal ingeweza kusajili walinzi sita ambao wamevihama vilabu vyao katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Kostas Manolas – Olympiakos kuelekea Roma £10m
Ezequiel Garay – Benfica kuelekea Zenit St Petersburg £5m
Mehdi Benatia - Roma kuelekea Bayern Munich £21m
Dante – Borussia Monchengladbach kuelekea Bayern Munich £4m
Ron Vlaar – Feyenoord kuelekea Aston Villa £3m
Eric Dier – Sporting Lisbon kuelekea Tottenham £4m
No comments:
Post a Comment