KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 15, 2014

JOHN MIKEL OBI AMTOLEA LUGHA CHAFU YA KARAHA MWANDISHI WA KIKE NCHINI NIGERIA

Mikel John Obi matatizoni kwa lugha chafu dhidi ya mwandishi wa kike nchini Nigeria
NYOTA wa Chelsea na timu ya taifa ya Nigeria John Obi Mikel amelaumiwa kwa kumtolea lugha chafu isiyofaa hadharani mwandishi mmoja wa kike ambaye alimuomba kiungo huyo kufanya naye mahojiano wakati akitoka mazoezini kujiandaa na mchezo wa kimataifa akiwa na kikosi cha Nigeria.
Mikel alikuwa akiondoka mazoezini baada ya mazoezi hayo kumalizika ambapo alifuatwa na mwandishi huyo wa kike anayefanyia kazi katika kituo kimoja cha redio cha KISS FM mjini Abuja.
Mwandishi huyo amekaririwa akisema alimuuliza kiungo huyo wa Chelsea kama watapata nafasi ya kuzungumza naye juu ya mchezo ujao wa kimataifa ndipo Mikel alipotoa maneno hayo ya karaha kwa mwandishi huyo.
Taarifa hiyo imeripotiwa kwa kina na mtangazaji BBC Oluwashina Okeleji, ambaye amesema tangu wakati huo mwandishi huyo aliamua kumsamehe Mikel kwa tukio hilo.
Hii si Mara ya kwanza ndani ya wiki hii ambapo iliripotiwa kuwa Mikel aliingia matatizoni na vyombo vya habari ambapo mwandishi mwingine wa habari Colin Udoh aliandika kupitia ukurasa wake wa kijamii wa twitter kuwa alitolewa maneno machafu na kiungo huyo alipokuwa akifanya naye mahojiano.