Kwa hisani ya EA Sports Player Performance Index, Rockersports inaweka wazi ni wachezaji gani wameonyesha soka la juu katika kipindi cha miezi miwili tangu kuanza kwa msimu wa ligi kuu ya soka nchini England.
Kama inavyodhaniwa na wengi ni Chelsea ambayo kwasasa inakalia usukani wa msimamo wa ligi soka nchini England 'Premier League' ikishinda michezo sita katika michezo yao saba ya ufunguzi wa ligi ambayo inawachezaji watatu wanang'ara katika orodha ya wachezaji walio katika kiwango cha juu yaani 'Player Performance Index rankings'.
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa amekuwa ni mchezaji aliyeizoea ligi ya England haraka akiwa katika moto wa hali ya juu
EA PPI Ranking | Player | Team | EA PPI Score |
---|---|---|---|
1 | Diego Costa | Chelsea | 287 |
2 | Eden Hazard | Chelsea | 188 |
3 | Cesc Fàbregas | Chelsea | 176 |
4 | Raheem Sterling | Liverpool | 172 |
5 | Gylfi Sigurdsson | Swansea City | 168 |
6 | Sergio Agüero | Manchester City | 166 |
7 | Graziano Pellè | Southampton | 161 |
8 | Saido Berahino | West Bromwich Albion | 161 |
9 | Morgan Schneiderlin | Southampton | 159 |
10 | Leonardo Ulloa | Leicester City | 158 |
Mfungaji anayeongoza Diego Costa, ambaye amefunga magoli tisa tangu kujiunga na Chelsea akitokea Atletico Madrid kiangazi , anaongoza katika chati hiyo akifuatiwa na wachezaji wenzake wa Chelsea Eden Hazard na Cesc Fabregas ambao ambao wameisaidia Hispania mara nne.
Raheem
Sterling, ambaye alitokea benchi katika mchezo wa ushindi wa England dhidi ya Estonia Jumapili, yuko katika nafasi ya nne katika chati hiyo ya ubora ya PPI akipata kura 172 na kufuatiwa na kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson mwenye kura 168 na mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero akifuatia kwa kura 166.
No comments:
Post a Comment