Baada ya Arsenal kupiga hatua moja mbele na kukaribia kukamilisha usajili wa kiungo Sami
Khedira baada ya Real Madrid kukubali kufungua mazungumzo ya kusajili mbadala wake.
Washika mitutu wanadhaniwa wamekubali kimsingi juu ya vipengele vinavyomuhusu mchezaji mwenyewe kwa maana ya Khedira ikiwa kusafisha barabara ya kujiunga na Emirates Stadium, ambapo sasa ada ya uhamisho ikiwa ndio mjadala ulioko mezani ukijadiliwa na pande mbilo hizi.
Na kinachoonekana ni kama kumalizia taratibu tu yaani kufuata njia ya halali ambapo gazeti la Marca limeripoti kuwa Arsenal watakuwa huru kumchukua Khedira endapo Madrid watafanikiwa kumnasa nyota wa Cruziero Lucas Silva.
Huyu ni Lucas Silva wa Cruziero ya Brazil ambaye endapo atasajiliwa tu na Madrid basi Sami Khedira ni mali ya Arsenal |
Madrid wameanza mazungumzo juu ya namna ya kumpata Silva na wamamatumaini kuwa kiasi cha pauni milioni £15 walichotenga kwa ajili ya Silva kitakubaliwa na kwamba hiyo ni fursa kwa Khedira kujiunga na Arsenal.
No comments:
Post a Comment