KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 15, 2014

Dawa ya safu ya ulinzi ya Arsenal anayo Mats Hummels wa Dortmund sasa ananukia Emirate mwenzi Januari

Huenda akatua Emirate
Arsenal wako tayari kuanza mazungumzo na Borussia juu ya mpango wa kumsajili mlinzi wa kati Mats Hummels wakati wa uhamisho wa mwezi januari.

Washika mitutu wamekuwa wakisumbuliwa na makosa ya eneo la ulinzi katika misimu ya hivi karubini na inaelezwa kuwa klabu hiyo ina pesa ya kutosha kufanya usajili mwezi Januari na pendekezo lao la kwanza ni Hummels.

Taarifa nchini Hispania zinasema Wenger ameamua hilo wiki hii na kudai kuwa Hummels ndiye mtu wa kutatua shida ya eneo la ulinzi na kwamba sasa yuko tayari kuanza mazungumzo na Dortmund juu ya mpango huo.

Mlinzi huyo wa kimataifa wa Ujerumani alidokeza huko nyuma kuwa anataka kusalia Dortmund mpaka kustaafu lakini Arsenal inaonekana ina nguvu ya kumshawishi mlinzi huyu kifedha na kumpeleka London ya Kaskazini.
Hapa Hummels anapongezwa na mpenzi wake baada ya mchezo wa fainali ya kombe la dunia nchini Brazil

No comments:

Post a Comment