KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 15, 2014

Mahaba niueee: Goli la Graziano Pelle wa Italia dhidi ya Malta lavuta hisia za mapenzi kwa mpenzi wake mwanamitindo Viky Varga

Graziano Pelle tunaweza kusema kuwa yuko ON FIRE katika ufungaji wa magoli kwa hivi sasa akianzia katika klabu yake ya Southampton mpaka katika kikosi cha timu ya taifa ya Italia.
Anafanya hivi kutokana na pengine kupata faraja kutoka kwa mpenzi wake Viky Varga.
Mshambuliaji huyo wa Southampton alifunga goli pekee la Italia katika mchezo wake wa kwanza wa kimataifa Jumapili wakati kikosi cha timu ya taifa ya Italia chini ya kocha Antonio Conte kilipo pata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Malta mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu mataifa ya Ulaya 2016.
Mpenzi wake mwana-mitindo mrembo kutoka nchini Hungary alishangilia goli hilo kwa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, ambako alitupia picha yenye ishara ya upendo na mahaba makubwa wakiwa wawili wamekumbatiana ikiambatana na ujumbe 
'Distance means so little when someone means so much.'
Viky Varga congratulates her partner Graziano Pelle on his winning strike for Italy via Instagram
Viky Varga akimfurahia mpenzi wake Graziano Pelle kwa goli la ushindi la Italia kwa kutupia picha yao wakiwa wamekumbatiana ndani ya mahaba mazito kupitia ukurasa wake wa Instagram
Pelle celebrates scoring his first Italy goal away to Malta, which handed Antonio Conte's side all three points
Pelle akishangilia goli lake la kwanza dhidi ya Malta, ambalo alimeipa ushindi kikosi cha Antonio Conte alama zote tatu
Pelle was mobbed by his team-mates as he took his superb form for Southampton to the international stage
Pelle akikusanya kijiji wakimpongeza kwa kufunga goli Jumapili ikiwa ni baada ya kuwa katika kiwango kizuri kiuchezaji akiwa na Southampton na sasa akifanya hivyo katika timu ya taifa ya Italia