KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, October 11, 2013

Matokeo ya michezo ya soka nchini Hispania yananuka rushwa, uchunguzi wabaini mechi mpaka kumi kuhusishwa na rushwa.

Rais wa ligi za soka nchini Hispania Javier Tebas amesema kuwa anagalau michezo nane ya ligi mbili za juu nchini humo zinapangwa matokeo yake.
Akiongea na kipindi kinachorushwa na shirika la utangazaji la nchini England BBC's World Football Show Tebas pia ametaka adhabu itolewe kwa wale wanaohusika na upangaji huo wa matokeo.
Amenukuliwa akisema
"Kati ya ligi ya daraja la kwanza na daraja la pili kiasi kama michezo minane mpaka kumi matokeo yake yanachakachuliwa kwa msimu.
"Endapo haitachukuliwa hatua haraka athari yake itakuwa kubwa"

Tebas, ambaye ni kiongozi wa ligi hizo mbili pia amewaambia wakuu katika mkutano wa kandanda (Football conference) mjini London, kupitia mkalimani kuwa anaamini tatizo kubwa limeletwa na wahuni wa kimataifa(international mafia).

Uchunguzi(Investigation)

Chombo hicho cha kusimamia ligi nchini Hispania kilifanyia uchunguzi mchezo wa ligi ambao Deportivo La Coruna ilishinda bao 4-0 dhidi ya Levante mwezi April mwaka huu 2013 baada ya Javier Barkero kuripotiwa na vyombo vya habari kuwashutumu baadhi ya wachezaji wenzake wa Levante kutokujaribu kufunga.

"Ina leta maana kwa wachezaji wenye matatizo ya kifedha kurubuniwa lakini hatuwezi kuchukua hilo kwa ujumla wake"

akaongeza kwa kusema 
"Intokea pia kwa wachezaji ambao wanapata pesa nyingi na ambao wako vizuri lakini najaribu kuondoa uchafu huu katika La Liga. 

"Kama hatuta liondoa hili sasa itakuwa ni kama Wild West bila ya sheria na bila ya udhibiti"
Mwezi Mei , Rais wa Deportivo La Coruna Augusto Cesar Lendoiro alidai kuwa udanganyifu wa matokeo ya mchezo umezidi kuwa mkubwa katika soka nchini Hispania baada ya chama cha ligi ya Hispania (Spanish Football League) kusema kuwa kilikuwa kikichunguza ushindi wa timu yake dhidi ya Levante wa mwezi April.

No comments:

Post a Comment