KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, October 11, 2013

ROONEY ALETA KIZUNGUMKUTI KINGINE CHA KUGOMEA MKATABA UNITED

Wayne Rooney amegomea kuanza mazungumzo ya mkataba wake mpya na Manchester United.
Licha ya kutoa kauli wiki hii kuwa yuko furahani na ametulia sasa Old Trafford, mshambuliaji huyo bado anaendeleza wasiwasi juu ya uwezekano wa kuondoka ndani ya klabu hiyo.
Imefahamika kuwa kambi ya Rooney imegomea wito wa wakuu wa United wa kuanza mazungumzo ya kuongeza mkataba wake ambao unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao.

Mshambuliaji huyo ambaye anatarajiwa kufikisha umri wa miaka 28 baadaye mwezi huu wa Oktoba, ameanza msimu kwa kiwango kizuri lakini yuko tayari kuondoka kwa mabingwa hao wa soka wa England (Premier League champions) na huenda ikwa mapema mwezi januari.
Rooney inaaminiwa kuwa kwasasa anasaka changamoto mpya katika klabu ambayo imejiweka vizuri katika ligi ya mabingwa Ulaya ambako hadhi yake ya kuwa mshambuliaji wa kati aliyeimara haitakuwa na maswali.
Kwasasa Rooney amekuwa mtulivu baada ya kukabidhiwa namba 10 na kocha mpya David Moyes tofauti na hali ilivyokuwa chini ya Sir Alex Ferguson aliyejiuzulu.
Akiongea Jumatano kuelekea katika mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Montenegro katika uwanja wa Wembley hii leo usimu, Rooney alitoa maneno ya kuwafariji mashabiki wa United kuwa atasaini mkataba mpya.
Alipoulizwa moja kwa moja endepo atasalia alijibu Rooney kwa kusema,

 "You can see I'm playing and I'm happy in my football. I'll have more discussions with the club and we'll see what happens from there."

No comments:

Post a Comment