UINGEREZA YAPATA PIGO LA MWANARIADHA NYOTA KATIKA MICHUANO YA MADOLA KUJITOA -NI MSOMALI RAIA WA UINGEREZABingwa mara mbili katika michuano ya riadha ya ulaya Mo Farah ametangaza kujitoa katika michuano mikubwa duniani ya jumuiya ya madola mwaka huu wa 2010 kutoka na kile kilecho elezwa kuwa ni kuchoka kwa mwili wa mwanariadha huyo”fatigue”.
Mwanariadhaa huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye amewahi kushinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 5000 za Great Britain na mbio za mita 10,000m katika michuano ya riadha ya mwaka huu wa 2010 za European Championships kule Barcelona anasema anahitaji kupumzika.
Farah ambaye alivunja rekodi ya mbio za mita 5000 za British mwezi August alikuwa aiwakilishe Uingereza katika mbio zote mbili michuano ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake katika jiji la Delhi mnamo October 3.
Akikaririwa anasema
"My body is telling me it is time to take a break."
Mwanariadha huyo ambaye kiasili ni msomali amekuwa katika mafanikio mwaka huu baada ya kumshinda Briton Chris Thompson katika mbio za Ulaya za mita 10,000 kabla ya siku nne baadaye kutwaa medali nyingine ya dhahabu za mita 5,000m .
No comments:
Post a Comment