KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, September 4, 2010

ENGLAND YAANZA VIZURI HUKU UFARANSA IKIPATA MSHITUKO KUFUZU EURO 2012 DEFOE APIGA HAT-TRICK LICHA YA MAUMIVU England imeanza vizuri kampeni zake za kufuzu fainali ya mataifa ya Ulaya maarufu kama Euro 2012 kwa ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Bulgaria,wakati ambapo kocha wa kikosi cha timu ya taifa ya ufaransa Laurent Blanc akiwa katika mchezo wake wa kwanza akipata mshituko baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 toka kwa Belarus na Ureno wakishikiliwa vizuri na Cyprus katika mchezo ambao umezaa jumla ya mabao manane . wakati hayo yakiwa hivyo Hispania mabingwa wa kandanda dunia wakiikandamiza Liechtenstein kwa jumla ya mabao 4-0 na Italy iliyokuwa nyuma ikipata ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Estonia.
Uingereza vs Bulgaria
Jermain Defoe aling’ara katika mchezo huo kwa kuonyesha makali ya kisu cha upasuaji kwa kufanikisha ushindi huo mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Bulgaria huku yeye pekee akifanikiwa kufunga jumla ya mabao matatu yaani “hat-trick”na kupeleka tabasamu katika sura ya kocha Fabio Capello.
Defoe ambaye aliahirisha kufanyiwa upasuaji kutokana na kusubiri mchezo huo sasa amefanikisha kupata jumla ya mabao 15 ndani ya michezo 44 aliyoitumikia timu ya taifa ya uingereza huku bao lingine la mchezo huo likungwa na Adam Johnson
.


Ujrumani vs Belgium
Miroslav Klose amefanikisha kampeni kuanza vizuri kwa upande wa ujerumani na kuipa ujerumani ushindi wa bao 1-0 na kuanza vizuri kampeni hizo,close amefunga bao hilo katika dakika ya sita ya kipindi cha pili.

Italia vs estonia
Italy walikuwa nyuma kimatokeo wamefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Estonia na hivyo kumpa faraja kocha wao mpya Cesare Prandelli akipata ushindi wa kwanza wa kimashindano. Estonia waliokuwa wenyeji ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Sergei Zenjov kunako dakika ya 29 minutes huku mabao ya Azzurri yaifungwa na Antonio Cassano dakika ya 59 na Leonardo Bonucci dakika ya 62.

Ureno vs Cyprus
Andreas Avraam wa Cyprus katika mchezo huo ndiye aliyekuwa shujaa baada ya kuziba matumaini ya Ureno kupata ushindi katika mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu fainali za Euro 2012 katika mchezo uliopigwa in Guimaraes mchezo ambao umemalizika kwa sare ya mabao mengi 4-4.
Mabao ya Ureno yakifungwa na Hugo Almeida, Raul Meirele, Miguel Danny na Miguel Fernandes huku kwa upande wa Cyprua yakifungwa na Efstathios Aloneftis, Michael Constantinou, yiannis okkas na Andreas Avraam
Ufaransa vs belarus
Laurent Blanc katika mchezo wake wa kwanza wakimashindano akajikuta akipata mshituko kwa kupokea kichapo cha bao 1-0 toka kwa Belarus bao ambalo limefungwa na Sergey Kisliak dakika nne tu baada ya mchezo kuanza na hivyo kuanza kuweka matumaini ya ufaransa kufuzu katika fainali hizo katika mashaka licha ya kwamba ni mapema.
Katika mchezo huo Ufaransa ilishindwa kabisa kutawala mchezo

Hispania vs liechtenstein
Mabingwa wa dunia Hispania wameanza vizuri kutete taji lao la ulaya baada ya ushindi mnono wa mabao 4-0 katika mchezo uliochezwa Vaduz nyumbani kwao Liechtenstein huku mabao ya washindi yakifungwa na Fernando Torres aliyefunga mabao mawili, David Villa na David Silva
.
Italia vs estonia
Italy walikuwa nyuma kimatokeo wamefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Estonia na hivyo kumpa faraja kocha wao mpya Cesare Prandelli akipata ushindi wa kwanza wa kimashindano. Estonia waliokuwa wenyeji ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Sergei Zenjov kunako dakika ya 29 minutes huku mabao ya Azzurri yaifungwa na Antonio Cassano dakika ya 59 na Leonardo Bonucci dakika ya 62.
Ujrumani vs Belgium
Miroslav Klose amefanikisha kampeni kuanza vizuri kwa upande wa ujerumani na kuipa ujerumani ushindi wa bao 1-0 na kuanza vizuri kampeni hizo,close amefunga bao hilo katika dakika ya sita ya kipindi cha pili.
Uholanzi vs San Marino

hat-trick ya Klaas-Jan Huntelaar,bao la penalty la Dirk Kuyt na bao la dakika ya mwosho ya mchezo la kwake Ruud van Nistelrooy yameisaidia uholanzi kuanza vizuri kampeni zake dhidi ya San Marino kwa kupata ushindi wa mabao 5-0. Bao la Van Nistelrooy limemfanya sasa kufikia rekodi ya Patrick Kluivert ya kufunga jumla ya mabao 40 kwa kuifungia uholanzi kimataifa.
Russia vs Andora
Mshambuliaji Pavel Pogrebnyak akifunga mabao mawili kwa upande wa timu yake ya taifa ya Russia mabao ambayo yameisaidia Russia kuanza vizuri kampeni kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Andorra. Bao la kwanza la Pogrebnyak limetokana na pasi murua ya Andrei Arshavin kunako dakika ya 14 na bao la pili ni kwa njia ya mkwaju wa penalty kunako dakika ya 65 baada ya kiungo mchezeshaji Alan Dzagoev kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.
Republic of Ireland vs Armenia

Bao la Keith Fahey aliyetokea bench lilizindua kampeni za mapema kwa jamhuri ya Ireland kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Armenia. Kiungo huyo wa Birmingham amefunga bao lake la kwanza kimataifa katika dakika ya 76 ya mchezo

No comments:

Post a Comment