Mchezaji wa zamani wa timu ya
Manchester United Roy Keane amesema kuwa aliyekuwa kocha wa kilabu hiyo
alikosea kuwashtumu wachezaji wake wa zamani katika wasifu wake na kwamba
haogopi kumkaripia iwapo wawili hao watakutana.
Ferguson
alizungumzia kuhusu wachezaji wa zamani wa kilabu hiyo Roy Kea na david Beckam
katika kitabu hicho kilichochapishwa mwaka uliopita.Keane aliondoka Old
trafford mwaka 2005 baada ya kukosana na Fergurson.
''Nahisi ni
makosa makubwa kunishtumu mimi na wachezaji wengine'' Keane mwenye umri wa
miaka 43 aliambia Footbal Focus.''tulifanya vyema katika kilabu hiyo ,tuliweza
kupata mafanikio ,tulishinda mataji na sasa kocha anatushtumu.
''Meneja
ambaye amejipatia mamilioni ya pauni kutokana na jasho letu,alikabidhiwa sanamu
na maeneo yaliotajwa baada ya jina lake, na anafikiri anaweza kutushtumu bila
mmoja wetu kusema lolote kwa kuwa anadhani ana mamlaka yote.
Nilisema
haiwezekani,kwa nini tukubali kusikiza upuzi kama huu.katika kitabu chake
Fergurson amedai kwamba Roy Keane ambaye alikuwa kiungo muhimu wa mafanikio ya
timu katika miaka 12 aliyoichezea aliendelea kuwa na ushawishi mbaya.
Keane
amesema kuwa hadhani kuwa anaweza kumsamehe Fergurson kwa matamshi yake na
kuongezea kwamba hajali kusema lolote lililo moyoni mwake kwa meneja huyo wa
zamani iwapo watakutana tena.
Laurent Koscielny naye apata majeraha na kuongeza maumivu kwa Arsene Wenger
Bundi wa majeraha ameendelea kudumu
katika klabu ya Arsenal kufuatia beki Laurent Koscielny kulazimika kujiondoa
kwenye mazoezi ya timu yake ya kitaifa ya Ufaransa kutokana na maumivu ya ukano
wa kisigino.
Meneja
Arsene Wenger amepigwa na pigo moja baada ya lingine ikiwa ni mechi saba tu
ndani ya msimu mpya huku ambapo sasa Koscielny anajiunga na nyota wenzake
Mathieu Debuchy, Mikel Arteta, Olivier Giroud, David Ospina, Aaron Ramsey na
Yaya Sanogo kwenye zahanati.
Siku mbili
baada ya Ujerumani kutangaza kiungo nyota Mesut Ozil atalazimika kutocheza kati
ya wiki 10 na 12, Wenger ameongezewa tumbo joto na habari kuwa beki Koscielny
amejiondoa kutoka mechi za Ufaransa dhidi ya Ureno na Armenia kwenye msururu wa
kufuzu Kombe la Euro la 2016.
Shirikisho
la Ufaransa limeandika kwenye anwani yao ya mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa
Koscielny anauguza uvimbe wa ukano wake wa kisigino.
Frank Ribery kurejea uwanjani hivi karibuni
Mshambuliaji Franck Ribery anakaribia
kurejea katika klabu yake ya Bayern Munch kufuatia kukosekana kwa kipindi
kirefu.
Nyota huyo
wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa ameichezea klabu yake mchezo mmoja tuu msimu
huu kufuatia kupata maumivu ya mguu.
Lakini hata
hivyo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye alilazimika kuikosa
michezo ya kombe la dunia wakati wa kiangazi nchini Brazil kutokana na maumivu
ya mgongo lakini sasa amerejea katika mazoezi baada ya kuponya matatizo ya
msuli yaliyokuwa yakimsumbua.
Taarifa
kupitia mtandao wa klabu yake imesema
"Franck
Ribery anaendelea vizuri kuelekea kurejea kikosini.
Bayern bado
wanaendelea kuikosa huduma ya Bastian Schweinsteiger, Thiago, Javi Martinez na Holger
Badstuber kutokana na kukumbwa na majeraha na hivyo kukipa kikosi cha kocha Pep
Guardiola wakati mgumu.
Kwasasa
Bayern inaongoza ligi kuu ya Ujerumani Bunderliga wakiwa mbele kwa zaidi ya
alama nne wakiwa na alama 17 baada ya michezo saba.
Arsene Wenger kupanga ratiba ya matibabu ya Ozil baada ya mchezo wa kimataifa wa Ujerumani
MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene
Wenger amesema watapanga ratiba ya matibabu ya Mesut Ozil baada ya kiungo huyo
kurejea kutoka katika majukumu ya kimataifa akiwa majeruhi.
Ozil
anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi mitatu kutokana na
majeruhi ya goti baada ya kufanyiwa vipimo akiwa na timu ya taifa ya Ujerumani.
Lakini
Wenger amesema mtaalamu wa klabu hiyo ndio atakaetoa ushauri wa jinsi gani ya
kukabiliana na tatizo hilo wakati watakapotafuta utaratibu wa kumtibu haraka
iwezekanavyo.
Wenger
aliendelea kudai kuwa madaktari wa Arsenal nao wataangalia vipimo alivyofanyiwa
na kutoa ushauri wao.
Arsenal imeandamwa na majeruhi kadhaa msimu
huu lakini Wenger amabinisha kuwa Theo Walcott na Serge Gnabry wote wanakaribia
kurejea katika kikosi cha kwanza wakati Aaron Ramsey naye amebakisha siku nane
kabla ya kuanza mazoezi.
Robert Pires amshauri Wenger kumununua Sami Khedira mwenzi Januari kwa kuwa ana vitu kama Patrick Viera
Robert Pires amemtaka Arsene Wenger kuwasha
tena moto wa mataji kwa Arsenal katika
ligi kuu ya England ( Premier League) kwa kumsajili Sami Khedira kutoka katika
klabu ya Real Madrid mwezi Januari.
Nyota huyo
wa zamani wa washika mitutu wa anaamini kuwa klabu yake hiyo ya zamani inakosa
kiungo bora mwenye sifa za aliyekuwa kiungo wakati wake Patrick Vieira.
Pires anaona
sifa zilezile za ufiti na kujituma ndani ya Khedira, ambaye alikuwa akihusishwa
kuelekea Arsenal wakati wa kiangazi ambaye sasa ameingia katika mwaka wake wa
mwisho wa mkataba na Madrid.
Amekaririwa
Pires akisema
“Wenger
anahitaji mchezaji wa kiungo mwenye mwili mkubwa kama Vieira, mwenye nguvu, mrefu,
kwasbaba nafasi hii ni muhimu kuunganisha ushambuliaji na ulinzi wa timu” Mfaransa
huyo alikuwa akionge na gazeti la Daily Telegraph.
“ubora upo, pengine mtu kama Yaya Toure katika
kiungo. Ananikumbusha Patrick Vieira, lakini pengine wanayo fursa hiyo hiyo kwa
Khedira.
Pires anaamini
timu ya Wenger bado wananafasi ya kuwania taji ingawa Chelsea ndio walioanza
vizuri msimu huku ikipata ushindi baina yao huko Stamford Bridge.
“wanazidiwa
na Chelsea kwa alama tisa lakini bado tunaweza kutwaa taji” Amesisitiza Pires.
Luis Saurez atakuwa nyota kuliko Messi na Neymar
Mshambuliji Luis Suarez ni mchezaji
ambaye atakuwa bora kuwazidi nyota wengine kama Lionel Messi na Neymar, hii
ni kauli ya mkongwe wa Uholanzi Johan Cruyff.
Suarez
aliyesajili wa kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £70 kiangazi kuelekea
Barcelona akitokea Liverpool bado hajaanza kutoa huduma katika klabu yake hiyo
mpya akiendelea na adhabu ya kusimama kwa miezi minne kufuatia kumtafuna Giorgio
Chiellini wa Italia wakati wa kombe la dunia.
Hata hivyo Cruyff
anasema Suarez ni habari nyingine na
tangu kutambulishwa Barcelona anamuona kama ni mtu ambaye ataamsha makali ya
safu ya ushambuliaji ya Barca.
Anasema
wakati wa kombe la dunia ni washambuliaji watatu ndio waliokuwa gumzo nchini
Brazil akiwemo yeye Suarez.
Amekaririwa
akisema
“Pengine
uwepo wa Suarez utaimarisha muunganiko mzuri kati ya Messi na Neymar,”.
“Pamoja na Messi,
wakati mwingine ni vigumu kufunga unahitaji usaidizi wa kufunga na Suarez ana
ubora huo, msimu uliopita hatukuona muunganiko hivyo tutaona nini
kitatokea baadaye.
Mchezaji wa kutumainiwa wa Guinea akimbia timu taifa kisa Ebola
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya
Guinea Alhassane Bangoura amefichua kwamba alijiondoa katika kikosi
kitakachokabiliana na timu ya taifa ya Ghana kwa sababu mchezaji mwenzake wa
timu ya Rayo Vallecano alihofia kwamba huenda akaambukizwa ugonjwa wa Ebola.
Mamia ya
watu tayari wamepoteza maisha yao kutokana na virusi vya ugonjwa wa Ebola
nchini Guinea hivyo basi taifa hilo limechukua hatua ya kuihamisha mechi yao ya
kufuzu kwa kombe la taifa bingwa barani Afrika nchini Morocco hapo jumamosi.
"Nilimuomba
mkufunzi wa timu ya taifa ya Guinea Michel Dussuyer kuniruhusu nijiondoe kwa
sababu wenzangu waliogopa kwenda,'' Bangoura aliiuambia mtandao wa Rayo.
''Rayo
haikuniambia chochote, maamuzi haya ni yangu binafsi''.
Mkurupuko wa
Ebola unaoshuhudiwa kwa sasa ktika eneo la Afrika Magharibi umewaua watu wengi
zaidi kuliko magonjwa mengine yote kwa pamoja, huku mataifa ya Guinea, Sierra
Leone na Liberia yakiathirika zaidi.
Kama njia
moja ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Ebola, shirikisho la kadanda nchini Sierra
Leone lilisitisha mechi zote za kadanda kufanyika.
Pia
shirikisho la kadanda la bara Afrika (CAF) liliamuru mechi zote zinazohusisha
timu za Sierra Leone, Guinea na Liberia zilizoratibiwa kuchezewa katika nchi
hizo kuhamishwa katika nchi nyingine tofauti
Sierra Leone
tayari imepata mataifa yatakayowaruhusu kuandaa mechi zake na wamewahakikishia
kwamba wameweka mikakati kabambe ya kuhakikisha ugonjwa huo hauambukizwi
wachezaji na wakufunzi.
Mataifa ya Afrika: Papiss Cisse kukiongoza kikosi cha Senegal dhidi ya Tunisia
Senegal inamatumaini mshambuliaji
wake anayechezea katika klabu ya Newcastle United Papiss Cisse atacheza kwa
kiwango cha juu kama anavyofanya katika ‘English Premier League’ watakapo ni wenyeji
wa Tunisia mjini Dakari.
Cisse alikuwa
bora katika mchezo uliomalizika kwa sare dhidi ya Swansea City wiki iliyopita
na kurejea kwake kutoka katika maumivu ya mguu itasaidia kujazia pengo loa
kukosekana kwa mshambuliaji mwingine wa Stoke City Mame Diouf, ambaye
anasumbuliwa na msuli wa paja.
Senegal
kwasasa ni moja kati ya timu za taifa ambazo zinamchezo mzuri barani Afrika
ikiwa na alama sita walizovuna katika michezo miwili dhidi ya Misri huku ambapo
nyota wa Lokomotiv Moscow Dame Ndoye akitoa mchango mkubwa katika kuzalishwa
kwa mabao.
Mabingwa
watetezi Nigeria watakuwa ugenini dhidi ya Sudan hapo kesho katika mchezo wa
kundi A wakisaka ushindi wa kwanza katika kundi baada ya kufungwa kwa mshituko
na Congo huku pia wakiwa na kumbukumbu ya sare dhidi ya Afrika kusini.
No comments:
Post a Comment