Wakala
wa mchezaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo Jorge Mendes amesema
kuwa mchezaji huyo hana nia yoyote ya kurudi Manchester United.
Ronaldo,
29, alikaa kwa miaka sita Old Trafford katika uchezaji wake wa soka,
lakini hivi karibuni amekuwa akihusishwa na taarifa za kutaka kurejea
kwenye klabu hiyo.
Ripoti
katika vyombo kadhaa vya habari nchini uingereza vilisema kuwa dili
hilo lililkuwa limepngwa kukamilika katika usajili wa mwaka 2015,
kiasi cha kufikia mashabaiki wa united kutuma vipeperushi vya
kuashiria kuridhia mchezaji huyo ambaye ni kipenzi chao kurejea
klabuni hapo, na hivi karibuni mashabiki wa united walionekeana
kwenye uwanja wa El Madriga ambapo Real walishinda bao 2-0 mwezi
uliopita.
Ronaldo
ambaye anashikilia tuzo ya Ballo , amefunga magoli 13 katika michezo
sita ya La la liga msimu na kumuongezea kujenga uwezo zaidi.
Mendes
amesema kuwa mteja wake hana dalili za kuondoka kwenye klabu hiyo
yenye maskani yake Estadio Santiago Bernabeu, na wala hakuna klabu
yoyote ambayo imekwishapiga simu ikihitaji huduma ya mchezaji huyo.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Wayne Rooney ajitathimini upya na hasira zake
Nahodha
wa Manchester United na England Wayne Rooney amesema kwa sasa ni mtu
mzima, lakini amekuwa akitafakari ni namna gani ataweza kuzuia hasira
zake mchezoni.
Rooney,
mwenye umri 28, amekosolewa vikali baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu
katika mchezo wa ligi kuu soka England ambapo United iliibuka na
ushindi wa bao 2-1 dhid ya West Ham uwanjani Old Trafford mwezi
uliopita.
Rooney
amesisitiza kuwa hivi sasa amebadilika tofauti na Yule wa zamani
ambaye alikuwa na tabia ya kukasirika kila mara, hivyo amewataka
radhi mashabiki wa united na kuongeza kuwa rafu aliyomchezea Stewart
Downing haikuwa ya kiungwana.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Mchezo wa AFCON wa Ghana dhidi ya Guinea kuchezwa Tamale
Chama
cha soka cha nchini Ghana GFA, kimeamua mchezo wake wa AFCON 2015
kati ya Ghana na Guinea
kuchezwa Tamale na si mjini Kumasi.
Rais
FA nchini Ghana Kwesi Nyantakyi amekanusha tetesi zilizodai kuwa
mchezo huo umehamishwa kutokana mapokezi hafifu ya mashabiki mjini
Kumasi katika mchezo wa Ghana na Uganda uliofanyika katika mji huo,
lakini ni utaratibu ambao wamejiwekea kwa ajili ya kuhakikisha miji
yote inashuhudia mechi za kimataifa.
Katika
upande mwingine Kwesi amesema kuwa nyumbani ni nyumbani, na uwanja wa
Kumasi haujatelekezwa moja kwa moja kwani wengine walishauri michezo
mingine ya Ghana kuchezwa Togo lakini Nyumbani ni Nyumbani.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Denis Oliechi kuungana na Harambee Stars
Mchezaji
wa kimataifa wa Kenya anaecheza soka la kulipwa nchini Ufaransa
Dennis Oliech hatoweza kujumika katika kikosi cha Harambee Stars
kitakachosafiri kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya
MOrroco utakaopigwa mjini Marrakech jumatatu ya October 13, 2014.
Kulingana
na kocha wa timu hiyo Bobby Williamson, Oliech, ambaye alikuwa nchni
Kenya kwa sababu binafsi yuko katika kambia kwa ajili ya kupasha
mwili joto na wenzake kwa nia ya kujiweka fiti.
Kocha
Bobby Williamson amekaririrwa akisema kuwa, Oliech yuko na wenzake
katika kambi ya timu ya tiafa ya Kenya lakini si mmoja ya wale
wataongozana na timu kuelekea nchini Morroco, lakini aliomba ruhusa
ya kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiweka fiti kabla ya kurudi katika
klabu yake hukio Ufaransa.
Oliech
kwa sasa hayuko katika mipangio ya kocha Williamson katika kikosi cha
sasa ila amempa nafasi ya kurudi kikosini katika majukumu mengione ya
kimataifa hususani kwenye michuano minine ya kimataifa.
Williamson
anataraji kukipunguza kikosi chake cha sasa kutoka wachezaji 26 mpaka
19 watakaondoka ijumaa, na watakaobaki watakuwa ni sehemu ya timu
hiyo.
@@@@@@@@@@@@@@
Diego Costa anasema yuko fiti
Diego
Costa ameonyesha kutosumbuliwa na tatizo lolote la maumivu ya misuli
ya paja baada ya kuanza mazoezi na timu ya Hispania kwa mafanikio ya
kujiandaa na michezo ya kufuzu kwa Euro 2016 dhidi ya Slovakia na
Luxembourg.
Msambuliaji
huyo wa Chelsea amejiunga na mchezaji mwenzake Cesi Fabregas
wanaotoka klabu moja, pamoja na nyota wengine wanoacheza ligi soka
England akiwemo David Silva na golikipa David de Gea wa Manchester.
Timu
hiyo inayofundishwa na kocha mkongwe Vicente del Bosque, iliitandika
Macedonia goli 5-1 katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo, na
sasa ni zamu ya Slovakia pamoja na Luxembourg.
Costa,
amefunga magoli tisa katika mechi saba za ligi kuu soka England,
akichezea klabu yake ya Chelsea msimu huu, lakini amekuwa na wakati
mgumu kupachika magoli akiwa na kikosi cha Hispania katika michezo ya
kimataifa hivyo ni wakati mwingine wa mchezaji huyo kuonyesha makali
yake katika michezo hiyo miwili ya juma hili.
Wakati
huo huo Kocha Del Bosque, amesema kuwa hashangazwi na timu yake
kushindwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika michuano ya kombe
la dunia huko Brazil, na kuongeza kuwa timu hiyo iko katika kipindi
cha mpito licha ya kupoteza muelekeo katika michuano hiyo mikubwa.
Hata
hivyo amewataka wachezaji wake kusahau yaliyopita huko Brazil, kwani
hivi sasa ana damu mpya ambazo zina ari ya kutaka kufanya makubwa, ni
bora wakawaza mwanzo mpya.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
No comments:
Post a Comment