KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 8, 2014

Mzee Hamisi Kilomoni ampa makavu Evance Aveva juu ya umuhimu wa wazee wa klabu ya Simba

Uongozi wa klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam umekumbushwa kurejea kwa wazee wa klabu hiyo ili kupata baraka za kuiongoza klabu hiyo ambayo kwasasa inaonekana imeanza kunyemelewa mgawanyiko mkubwa wa wanachama wake.
Akiongea na mtandao wa Rockersports nyota wa zamani wa klabu hiyo ambaye pia aliwahi kuwa katibu mkuu na mdhamini katika vipindi tofauti Hamisi Ally Kilomoni ameonekana kushangazwa na uongozi ulioko madarakani kwa sasa chini ya Rais Evance Aveva, kuwa umewasahau wazee wa klabu hiyo ambao wamepata shida na klabu hiyo katika vipindi mbalimbali vya uongozi wa klabu hiyo.
Kilomoni amesema huko nyuma haikuwahi kutokea kwa wanachama wa klabu hiyo kufukuzana uanachama jambo ambalo amesema endapo Aveva atashindwa kuwaita wazee wa klabu hiyo kupata muafaka wa wanachama waliotimuliwa basi huenda mambo yakaenda mrama katika uongozi wake.
Aidha amekanusha kulikumbatia kundi lililojitokeza hivi sasa maarufu kama 'UKAWA' ambalo linaonekana kuwa na joto la upinzani ndani ya klabu hiyo ambalo sehemu kubwa ya wanachama wake walitumuliwa na mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo kutokana na kuelekea mahakamani kupinga maamuzi ya kuenguliwa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi kwa Michael Wambura aliyekuwa mnpinzani wa Aveva.
Mzee Kilomoni ambaye aliondolewa katika nafasi ya udhamini wa klabu hiyo yeye na mzee Abdul Wahabu amesema pamoja na kwamba klabu hiyo inaongozwa na vijana ambao wanataka kuiongoza kisasa lakini bado kuna watu walio hai ambao wamepata tabu katika kuijenga klabu hiyo tangu zama za jina la Sunderland katika miaka ya 1960's tena kwa kuchangia fedha zao za mifukoni.
Bofya chini kumsikiliza mzee kilomoni

No comments:

Post a Comment