KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, October 12, 2014

Seydou Keita naye ajiunga katika orodha ya majera kikosini Roma

Kiungo wa Roma Seydou Keita

As Roma yapigwa na jinamizi la majeraha kufuatia kiungo Seydou Keita kupata majeraha makubwa katika mchezo wa kimataifa.
Kiungo huyo mahiri kabisa wa Mali alilazimika kutolewa nje katika dakika ya 30 hapo jana katika mchezo wa kuwani kufuzu mataifa ya Afrika dhidi ya Ethiopia na akikabiliwa na maumivu ya msuli.
Imeelelzwa kuwa bado ukubwa wa maumivu hayo haijajulikana.
Mwenyewe Keita kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter ameshukuru pole nyingi zilizotumwa kwake akisema "Thank you for all your messages of encouragement,I hope it is not a serious injury. I'll be back soon and stronger."
Maumivu ya Keita yanakuja wakati tayari wakiendelea kusubiri huduma ya Daniele De Rossi na Kevin Strootman ambao nao ni majeruhi.
Kwasasa mchezaji huyo wa Barcelona yuko katika kiwango kizuri katika kikosi cha kocha Rudi Garcia tangu alipojiunga nayo akitokea kwa mkataba wa mwaka mmoja akitoke katika klabu ya Valencia kiangazi.