KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, October 12, 2014

Caf yaitolea nje Morocco kuhusu mataifa ya Afrika

Shirikisho la soka barani Afrika, Caf limetofautiana na wenyeji Morocco ambapo wamesisitiza kuwa fainali za mataifa ya Afrika 2015 itaendelea kama ilivyopanga licha ya nchi andalizi kuelezea hofu ya ugonjwa hatari wa Ebola.
Morocco waliomba shindano hilo liahirishwa kufuatia mripuko wa ugonjwa huo ambao umeua watu zaidi ya 4,000 baada ya maafisa wa afya nchini humo kuonya kuendelea kwa fainali hizo kwa madai yanaweza kuendeleza uambukizaji zaidi.
Mshauri wa Waziri wa Michezo wa Morocco, Mohammed Ouzzine, alieleza taifa hilo la magharibi mwa bara hilo lina wasiwasi kuandaa shindano hilo linalochukua wiki tatu.
“Matakwa ya Morocco na wakaazi wake pamoja na wale wa bara Afrika yanadunisha linguine lolote. Morocco wamewasilisha ombi hilo kufuatia ushauri muhimu kutoka maafisa wa afya.
“Hatuwezi hatarisha maisha ya watu kwa kuendelea kuandaa shindano hili kwani msingi wa tahadhari unafaa kufuatwa,” mshauri Hamid Faridi aliambia stesheni ya redio, Atlantic Jumamosi.
Kwa majibu, Caf walitoa taarifa wakitofautiana na wenyeji hao huku Afrika Kusini wakilengwa kama waandalizi wa dharura ikiwa Morocco watajiondoa.
“Caf wanadhibitisha hakuna badiliko kwenye ratiba ya shindano hili. Tungependa kukumbusha kwamba tangu dimba la kwanza la 1975, shindano hili halijawahi chelewa au kuhairishwa,” taarifa ya utawala huo wa kandanda ilisema.
Mataifa ya Afrika magharibi, Guinea, Liberia na Sierra Leone yameadhirika zaidi na mkurupuko wa sasa wa Ebola. Guinea na Sierra Leone bado wanawania tiketi za Morocco 2015.
Afrika Kusini waliokoa jahazi la shindano hilo 1996 na mwaka jana.

No comments:

Post a Comment