KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, October 12, 2014

Jose Maourinho anajipima ni vipi atamng'oa Varane Real Madrid

Jose Maourinho ametanabaisha kuwa anaendelea kupendezwa na uchezaji wa Raphael Varane lakini akaweka wazi kuwa nafasi ni finyu kwa klabu yake ya Real Madrid kumuachia kujiunga na Chelsea.

Varane alianza kuichezea Madris iliyokuwa chini ya Mourinho Septemba 2011 na tangu wakati huo amejiimarisha kikosini katika nafasi ya ulinzi huku pia aking'ara zaidi katika fainali ya kombe la dunia nchini Brazil na sasa akiwa ni mlinzi tegemeo katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa.

Wakati bosi huyo wa Chelsea akidokeza kujaribu kutaka kumng'oa Varane Madrid, bado anaona ni vigumu kuondoka kwa mabingwa hao wa Ulaya.

"I Like Varane, but everybody knows that he will stay at Real Madrid," Mourinho alikuwa kiongea na Telefoot.