KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, October 12, 2014

Tanzania yaikamua Benin 4-1 iliyojaa nyota kibao kutoka Ulaya akiwemo Stephane Sessegnon wa West Bromwich Albion na Steve Mounie wa Montpellier ya Ufaransa

Mshambuliaji wa Tanzania Juma Luizio akiandika bao la nne la timu yake katika mchezo uliofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ambao Tanzania iliibuka na ushindi wa bao 4-1. Mabao mengine yalifungwa na Nadir Haroub, Amri Kinemba na Thomas Ulimwengu.

Kikundi kipya cha ushangiliaji kinachojizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania kwa sasa nacho kilikuwepo uwanjani kuishangilia Tanzania wakati wa mchezo dhidi ya Benin na Tanzania kuibuka na ushindi wa bao 4-1, kundi hili ni la mashabiki wa timu ya Simba linalotambulika kama kikundi cha ushangiliaji cha MPIRA NA MAENDELEO.

Mshambuliaji Thomas Ulimwengu wa timu ya taifa ya Tanzania akipongezwa na mshambuliaji mwenzake Juma Luizio baada ya kuandika bao la tatu la timu yake katika mchezo uliofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Tanzania iliibuka na ushindi wa bao 4-1.