KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, October 13, 2014

Mjerumani Bern Schuster aingia katika kinyang'anyiro cha ukocha Black Stars

Bernd Schuster yumo katika orodha ya makocha watano ambao wanawania nafasi ya ukocha wa timu ya taifa ya Ghana, hizi zikiwa ni taarifa za shirikisho la soka nchini la nchi hiyo.
Bosi huyo wa zamani wa Real Madrid hakufikiriwa kuipigania kazi hiyo kabla ya kujitoa kwa Patrick Kluivert katika mchakato huo kiasi kupelekea kuingia kwa mjerumani huyo katika orodha ya wapigania kazi hiyo.
Michel Pont na Marco Tardelli watakutana na FA ya Ghana Oktoba 17, kabla ya  Avram Grant na Juan Ignacio Martinez kufuatia siku itakayofuata wakati taifa hilo likiwa katika harakati za kusaka bosi mpya baada ya kuachana na James Appiah kwa hiari yake mwezi Septemba.
Appiah alikuwepo katika benchi katika kipindi cha miaka miwili na nusu na kukiongoza kikosi hicho kikienda sare ya bao 1-1 na Uganda mchezo wa kuwania kufuzu fainali ya mataifa ya Afrika na baadaye wakipata ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Togo