KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, September 9, 2013

JORDI ALBA ANATAKA KUWA MLINZI BORA WA KUSHOTO DUNIANI.

Mlinzi wa klabu ya Barcelona Jordi Alba amesema kuwa anatamani kuwa mlinzi bora wa kushoto duniani wakati kipindi chake cha kucheza soka kitakapo kuwa kinaelekea ukiongoni.

Mlinzi huyo mwenzi huyo ambaye alijiunga na Barcelona akitoke Valencia kiangazi mwaka jana amekuwa katika kiwango bora katika kipindi cha kuanza msimu wa 2013-14 ambapo pia ameonyesha matumaini ya kuboresha kiwango chake zaidi katika miaka ijayo.

Amenukuliwa akisema.
"Nataraji kuwa ni miongoni mwa walinzi bora duniani katika muda wangu wa kuelekea kumalizia muda wangu wa kucheza soka".

"Nafarijika watu wanapo nizungumzia kwa jinsi ninavyocheza vizuri lakini hiyo hainipi si kigezo kwangu kwasababu ni tofauti pale ninapocheza vibaya.

"Nina matumaini kuwa nazifi kukua kisoka na kwa miaka ijayo nitakuwa ni miongoni mwa wachezaji bora duniani"

Alba amefunga goli moja katika ushindi wa Hispania wa mabao 2-0 dhidi ya Finland Ijumaa na sasa akiwa amefanikiwa kufunga jumla ya mabao matano katika jumla ya mabao 24 aliyo ifungia nchi hiyo katika michuano ya Ulaya.

No comments:

Post a Comment