KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, September 9, 2013

GENNARO GATTUSO ANASEMA MASHABIKIWA MILAN WAMPE MUDA RICALDO KAKA.

Gennaro Gattuso amewataka mashabikiwa wa AC Milan kuwa wavumilivu na kumpa muda Ricaldo Kaka wakati huu ambapo kiungo huyo Mbrazil akiwa amejiunga na klabu yao na akitaka kuonyesha uwezo wa kucheza soka na kuonyesha miujiza yake ya soka mara baada ya kurejea ndani ya klabu hiyo akitokea katika klabu ya Real Madrid baada ya misimu minne ambayo hakuwa katika kiwango
 kizuri.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31alirejea Milan ambako alipoteza jina lake akisaini mkataba wa miaka miwili na klabu yake hiyo ya zamani katika siku ya mwisho huku bosi huyo wa sasa wa Palermo ambaye alikuwa kipenzi cha Rossoneri Gattuso akiwataka mashabiki wawe wavumilivu.

Ananukuliwa na Sky Sport Italia akisema 
"Lazima muwe wavumilivu na Kaka. Natumaini kuwa mashabiki hawako tayari kumuona Kaka yule wa zamani akipotea".

"Hatupaswi kusahau kuwa hakuwa akicheza sana kwa kipindi cha miaka mitatu na hakuwa katika kiwango chake cha juu.

"Ndio maana nasema mashabikiwa wa Milana wanapaswa kuwa wavumilivu na kumpa muda. Kaka ni mchezaji mzuri na na ni mtu mzuri kuwa naye katika chumba cha kubadilishia nguo."

Gattuso alikuwa katika kikosi kimoja na Kaka enzi hizo katika klabu ya Milan kuanzia 2003 mpaka 2009.

No comments:

Post a Comment